Mpiratz imehamia www.mpiratz.com

Tunapenda kuwajulisha wote kuwa, kuanzia sasa habari za http://www.mpiratz.wordpress.com zitakuwa zikitolewa katika tovuti yetu mpya ya www.mpiratz.com

 

Advertisements

LIVERPOOL WAMNASA HENRIKH

Henrikh Mkhitaryan

Henrikh Mkhitaryan

Klabu ya Liverpool yasemekana imefanikiwa kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Shaktar Donetsk Henrikh Mkhitaryan. Kocha wa Liverpool Rodgers yasemekana anavutiwa sana na uwezo wa kiungo huyo mwenye uraia wa Armenia mwenye umri wa miaka 24. Borussia Dortmund na Tottenham wote walikuwa na nia ya kumsajili kiungo huyo ila Liverpool ndio imeweza shinda mbio hizo. Yasemekana kiasi cha paundi mil 25 ndio kilichokubaliwa na Shaktar kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo.

Chanzo: Clubcall

Arsenal kumsajili Cesar wa QPR

Cesar

Cesar

Arsenal wanajipanga kukamilisha usajili wa kipa wa QPR Julio Cesar ambae kwa sasa yupo katika mashindano ya Confederations Cup.
Maongezi baina ya Cesar na Arsenal yameshaanza fanyika lakini kwa yasitishwa kwa muda mpaka mashindano hayo ya Confederations Cup yaishe.

QPR wapo tayari kupokea £2million kwa ajili ya Cesar ambaye kwa sasa anapokea £70,000 kwa wiki abako kwa arsenal haitokuwa tabu kumlipa.

Chanzo:Dailymail

Dawson na Vertonghen ndio walikuwa tofauti ya mchezo, Park ataiokoa QPR na Rooney kuichakaza Madrid

MUOKOZI: PARK JI-SUNG
Ushindi wa QPR ulipatikana kwa jitihada hasahasa za watu wawili ambao ni Jose Bosingwa na Park Ji-sung. Wote wamekuwa na mwanzo mbaya tokea wahamie QPR lakini katika mechi hii dhidi ya Sauthampton waliweza kung`aa na kuweza isaidia timu yao kuibuka na ushindi.Uzoefu wao wa kucheza katika mashindano makubwa kama Champions League ndio hasa uliowafanya waweze kung`ara.Tangu Park aihame Man UTD hii ndo mechi yake ya kwanza aliyoweza cheza katika kiwango kizuri, kiwango ambacho alikuwa akikionyesha pindi yupo United na kama akiendelea hivyo basi QPR yaweza nusurika na kushuka daraja msimu huu.

Park Ji-sung

Park Ji-sung

WALETE REAL…!!!
Rooney alifunga goli miongoni mwa magoli yaliyofungwa na United katika mechi dhidi ya Norwich na anatrajiwa kuwa mchezaji tegemeo dhidi ya Real hapo jumanne usiku. Jmabo la kufurahisha zaidi ni kuwa Welbeck alikuwa benchi katika mechi hiyo na kuleta dhana ya kuwa labda babu anataka kumtumia Welbeck kama silaha yake dhidi ya Real lakini sidhani kama ndo atakuwa mbadala wa Rooney au RVP.

Wayne Rooney

Wayne Rooney

KIJANA TOKA BRAZIL.
Philippe Coutinho ana miaka 20 tu na hana jina kubwa kama wabrazil wengine ambao wameshawahi pita au kuwika ila kijana huyu anamiguu mepesi na pia yenye kasi, aliweza wachachafya Wigan sana ingawaje sifa nyingi zimeenda kwa Suarez kutokana na hat-trick yake ila mie sifa zangu natupia kwa kijana Countinho, kwa kweli kama ataendelea hivyo na kujifunza mengine zaidi basi atakuja kuwa tishio mbeleni na kuweza iweka Liverpool mahala pazuri.

Philippe Coutinho

Philippe Coutinho

MABEKI WAWAOKOA SPURS.
Hata ukiiangalia mechi ya Arsenal na Spurs mara kumi bado utabaki na uamuzi mmoja ya kuwa beki ya Spurs ndio ilikuwa tofauti ya timu hizo mbili.Kama Michael Dawson na Jan Vertonghen wangekuwa wamevaa uzi mwekundu (jezi ya Arsenal) basi ninauhakika asilimia 120% Arsenal wangetoka na ushindi katika mechi hiyo dhidi ya watani wao wa jadi.

Michael Dawson

Michael Dawson


Jan Vertonghen

Jan Vertonghen

NEWCASTLE WAMSAJILI YANGA NA WATATU WENGINE KUFUATA.

yanga

yanga

Newcastle wamsajili nahodha wa Montpellier aitwaye Mapou Yanga-Mbiwa mchezaji huyo aliyekuwa anachezea soka lake nchini Ufaransa anajiunga na klabu hiyo na kupelekea wimbi la wachezaji watokao ufaransa kuongezeka klabuni hapo. Newcastle walimsajili Debuchy wiki iliyopita ambaye pia ametokea Ufaransa si hilo tu bali timu hiyo tayari imeshakamilisha maongezi na wachezaji wengine wawili (Gouffran,Massadio Haidara) ambao wote wanatokea ufaransa.
yanga vipimoni

yanga vipimoni


Chanzo: Dailymail

BRADFORD WAWATOA VILLA NA KUIGIA FAINALI WEMBLEY.

bradford wakishangilia ushindi.

bradford wakishangilia ushindi.

Bradford timu ambayo ni ya daraja la chini huko nchini Uingereza imeweza fanikiwa tinga fainali ya carling cup (wembley) baada ya kuitoa timu ya A.Villa lakini sio Villa tu ambao wameonja kipigo cha timu hiyo ndogo bali hata Arsenal na Wigan wote walipewa kichapo na timu hiyo.
bradford

bradford


Bradford ni timu ambayo jumla ya wachezaji wake wote kwa pamoja wamenunuliwa kwa kiasi cha paundi 7,500 tu, tofauti na gharama wanazo tumia akina Arsenal, Wigan na hata Villa.
wee refa shangiliaaaaaa...

wee refa shangiliaaaaaa…


Aston Villa: Given, Lowton, Vlaar, Clark, Bennett (Weimann 70), Ireland, Delph, Bannan (Bent 62), N’Zogbia, Benteke, Agbonlahor.
Subs not used: Guzan, Holman, Stevens, Lichaj, Carruthers.
weweeeeeeee....!!!1

weweeeeeeee….!!!1

\
wembleyyyyyyyy...

wembleyyyyyyyy…


Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good, Hines (Thompson 71), Gary Jones, Doyle, Atkinson, Hanson, Wells (Turgott 87).
Subs not used: McLaughlin, Ravenhill, Reid, Connell, Nelson.
duuuuh.....

duuuuh…..

Timu ya Bradford na gharama zake.
Matt Duke (Age 35)
Gharama ya usajili:Bure

Rory McArdle (Age 25)
Gharama ya usajili:Bure

Carl McHugh (Age 19)
Gharama ya usajili:Bure

Curtis Good (Age 19)
Gharama ya usajili:Bure

Zavon Hines (Age 24)
Gharama ya usajili:Bure

Nathan Doyle (Age 26)
Gharama ya usajili:Bure

Gary Jones (Age 35)
Gharama ya usajili:Bure

Will Atkinson (Age 24)
Gharama ya usajili:Bure

Nahki Wells (Age 22)
Gharama ya usajili:Bure

James Hanson (Age 25)
Cost: £7,500

Chanzo: Dailymail.

FERGIE AMTAKA WANYAMA.

WANYAMA AKIFUNGA GOLI

WANYAMA AKIFUNGA GOLI

FERGIE AKIWA GLASGOW.

FERGIE AKIWA GLASGOW.

Man United wakijiandaa na mechi ya FA dhidi ya Fulham wikiendi hii, kocha wao Sir Alex arudi kwao Scotland kwa ajili ya kumchunguza kwa karibu mchezaji wa CELTIC Victor Wanyama kwa ajili ya uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.
Wanyama mwenye umri wa miaka 21 amekuwa mchezaji muhimu wa Celtic msimu huu na kuweza kuifanya timu hiyo kuweza vuka hatua ya makundi ya UEFA.
Chanzo: DAILYMAIL

Chelsea 8 Aston Villa 0

chelsea..

chelsea..

Mwezi mmoja uliopita chuki na hasira dhidi ya uchaguzi wa Rafa Benitez ndio zilizokuwa zimetawala ndani ya Stamford bridge. Lakini jana mambo yalikuwa tofauti hakuna hata shabiki mmoja aliyeimba nyimbo za kumkebehi kocha huyo.

Torres 1-0.

Torres 1-0.

 luiz 2-0

luiz 2-0

ivanovic 3-0

ivanovic 3-0

lampard 4-0

lampard 4-0

Mara ya mwisho Chelsea iliposhinda magoli mengi namna hiyo ni pindi ilipokuwa ikifundishwa na Ancelotti dhidi ya Wigan. Lakini jana walikuwa chini ya Benitez kocha ambaye milele anachezesha wachezaji wake kwa tahadhari ya kufungwa.

ramires 5-0

ramires 5-0

oscar 6-0

oscar 6-0

hazard 7-0

hazard 7-0

ramirez 8-0

ramirez 8-0

Chelsea walicheza kwa umakini na pia tahadhari ya kutoruhusu goli kuingia nyavuni kwao. Torres ndie aliyefungua kapu la magoli akifuatiwa na Luis,Ivanovic,Lampard,Ramirez,Hazard,Oscar na mwishowe Ramirez akafunga goli lake la pili kwa mechi hiyo.

8-0..

8-0..

Chanzo: Dailymail

Gerrard kusaini mkataba mpya Liverpool.

Gerrard akifunga bao dhidi ya fulhamBrendan Rodgres yupo tayari kumpatia nahodha wake mkataba mpya pamoja na kuwepo na uvumi ya kuwa nahodha huyo kiwango chake kimeshuka.
Gerrard alifunga goli lake la pili la ligi kwa msimu huu dhihi ya Fulham. Katika mechi hiyo Gerrard ndiye alikuwa kinara kwa Liverpool kwa kuweza kufunga goli moja na kutengeneza mengine mawili. Rodgers anataka kumpa Gerrard mwenye umri wa miaka 32 mkataba mwengine ili aweze endelea wepo katika klabu hiyo zaidi na zaidi.

chanzo: The Times

Liverpool kumsajili Pohjanpalo.

Joel Pohjanpalo

Klabu ya Liverpool ipo mbioni kumsajili mshambuliaji wa HJK Helsinki aitwaye Joel Pohjanpalo.

Inasemekana Liverpool ilitaka msajili mchezaji huyo toka kipindi cha usajili lakini fikra hizo za kumsajili zimekuja tena na hivyo kuna uwezekano mkubwa akasajili katika dirisha dogo la Januari.

Rodgers..

Pohjanpalo mwenye umri wa miaka 18 inasemekana anafuatiliwa kwa karibu pia na klabu ya Borussia Monchegladbach lakini Liverpool ndio inapewa kipaumbele kwa inamshambuliaji mmoja wa kati tu mpaka sasa wa kueleweka (suarez).

Chanzo: Dailymail

Wachezaji wa Man City wajirusha katika shoo ya Nicki Minaj kabla ya mechi ya Ajax.

Mario Balotelli

Mario Balotelli na wenzake walienda nje ya jiji la Man City kwa ajili ya kujirusha katika shoo ya mwanamziki wa Hip Hop Nicki Minaj.

Micah Richards na James Milner

Wachezaji kama Balotelli, Joe Hart, Barry, Micah Richards na Lescott.

Joe Hart

Man city wanajiandaa kukutana na Ajax baada ya kuanza vibaya katika mashindano hayo ya Uefa kwa kufungwa mechi ya kwanza na Madrid na ya pili kutoa draw na Dortmund.

NICKI MINAJ

Chanzo: Dailymail

Man United waandaa majina ya warithi wa Ferguson lakini yafungiwa katika droo.

majina ya makocha kumrithi ferguson yafungiwa katika droo

United wamesema ya kuwa mipango ya kuandaa mbadala wa Ferguson imeshaanza kufanyika na majina ya makocha hao ambao ni mbadala yameshachaguliwa na yamefungiwa katika droo.

Jose Mourinho

David Moyes

Mwenyekiti msaidizi wa Man United Ed Woodward amesema ya kuwa majina ya makocha wa kumrithi Ferguson tayari yameshachaguliwa ingawa tarehe rasmi ya Ferguson ya kustaafu bado haijajulikana.
“tumeshajiandaa na tayari tunajua ni kivipi tutafanya mipango yetu ili kuweza mpata kocha ingawa majina ya hao makocha wote yapo katika droo na yatabakia humohumo”.

Pep Guardiola

Majina ya makocha ambao yanafikiriwa kuwepo katika droo ni ya Jose Mourinho, Pep Guardiola na David Moyes.

Chanzo: Dailymail

ENGLAND WABAGULIWA SERBIA.

Timu ya Uingereza ya U21 jana ilikuwa inacheza na timu ya Serbia na kuweza kufanikiwa kutoka na ushindi wa mabao mawili kwa bila (2-0). Lkini ushindi huo uliambatana na ugomvi wa hali ya juu uliosababishwa na ubaguzi wa rangi waliofanyiwa wachezaji wenye rangi nyeusi wa Uingereza. Mtusi, ngumi na mateke yote yalitumika.

UGOMVI UKIANZA

DANNY ROSE AKIRUDISHA MASHAMBULIZI YA UBAGUZI BAADA YA KUPEWA RED CARD

mshikemshike

kocha Martin Thomas wa uingereza akipigwa kichwa na kocha wa Serbia

kocha Steve Wigley wa uingereza akivamiwa

huniambii kitu wewe

sheenzi

inatosha jamaniiiii!!

Chanzo: Dailymail

 

 

 

 

 

 

 

 

Sat 22 Sep 2012 – Premier League

Sat 22 Sep 2012 – Premier League

Swansea 0 – 3 Everton
Chelsea 1 – 0 Stoke
Newcastle P – P Norwich

Southampton 4 – 1 Aston Villa
West Brom 1 – 0 Reading
West Ham 1 – 1 Sunderland
Wigan 1 – 2 Fulham

Man United kumuuza Nani kwa Zenit…?

Nani

Mchezaji wa timu ya Manchester United Nani anasubiri kujua hatima yake leo kama atauzwa na United kwenda klabu ya Zenit St Petersburg kabla dirisha la Usajili la Urusi halijafungwa leo.

WITSEL

Zenit wameushangaza ulimwengu wa soka baada ya kutoa paundi mil 70 kwa ajili ya kuwasajili mshambuliaji wa Porto Hulk na kiungo wa Benfica Axel Witsel na inasemekana wanataka toa paundi mil 25 kwa ajili ya kumpata Nani.

Hulk

Vilevile inasemekana Zenit wanataka kumrudisha Arshavin katika klabu hiyo kabla dirisha halijafungwa.

Andrey Arshavin

Nani alitarajiwa kusaini mkataba mpya na Man United ili aweze bakia klabuni hapo kwa mda mrefu lakini jambo hilo limeshindika kwani hapakuwa na maelewano mazuri katika mkataba huo na kupelekea Nani kujiona haitajiki klabuni hapo na pia  inasemekana hayupo katika mipango ya kocha Ferguson.

Chanzo: Dailymail

Hatimaye Henriquez atua United kwa paundi mil 4.

Angelo Henriquez

Hatimaye klabu ya Man United imekamilisha usajili wa mchezaji mwenye umri wa miaka 18 Angelo Henriquez.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Chile alifanyiwa vipimo tokea mwezi wa nane lakini hivi leo ndio ametambulishwa rasmi kama mchzaji wa Man United.

Angelo Henriquez

Mchezaji huyo alihamia United akitokea Universidad de Chile ambako alifunga magoli 11 katika mechi 17 katika msimu wa 2012 na kuisaidia timu yake kutwaa kombe.

“Angelo anauwezo mkubwa sana wa kimpira. Uwezo wake wa kukimbia na uwezo wake wa kuweza usoma mchezo ni mkubwa sana mpaka unashangaa uwezo wake ukilinganisha na umri wake.
Tuna sifika kwa kukuza vipaji na ninauhakika Angelo atakuja kuwa mchezaji bora sana.” alisema Ferguson.

Angelo Henriquez

“Ninafuraha sana na kujiunga na klabu kubwa duniani. Man United ni klabu kubwa na yenye kocha bora.
Kuweza kujiunga nao ni heshima kwangu na inanifanya ntake kujituma zaidi. Natarajia kutwaa vikombe vingi na klabu yangu hii mpya”. Alisema Henriquez.

Chanzo: Dailymail

Mancini amtaka Balotelli aache Sigara.

Mario Balotelli

Mchezaji wa Man City Mario Balotelli anamfanya kocha wake Roberto Mancini apate wasiwasi kutokana na tabia yake ya kuvuta Sigara tano kwa siku na hivyo kumuomba mchezaji huyo aende kwa daktari ili aweze iacha tabia hiyo.

Man City wanaamini uvutaji huo hautomsaidia Balotelli kuweza pona vizuri pindi atakapofanyiwa operesheni ya jicho wiki ijayo.

Msimu uliopita Mancini alimkatazaga Balotelli tabia hiyo ya uvutaji na kumshauri apunguze lakini kumbe mtukutu huyo hata hana mpango huo.

Mancini aliudhika zaidi pindi alipoona picha za Balotelli akivuta siku chache kabla hajafanyiwa operesheni.

Chanzo: Dailymail

Ferguson amruhusu Usain Bolt kuichezea United.

Sir Alex Ferguson na Usain Bolt

Sir Alex Ferguson amempa ruhusa Usain Bolt ya kuja kujiunga na kuichezea Man United katika mechi dhidi ya Real Madrid.

Mwanariadha huyo ambaye ndio bingwa wa mbio fupi duniani alimbembeleza Ferguson ampe nafasi na sasa Ferguson amemkubalia.

Bolt

“Usain ni mtu mzuri na shabiki mkubwa sana wa United.
Lakini cha ajabu zaidi ni pindi anaposema anataka kuichezea United katika mechi ya hisani (kuchangia hela ili kusaidia watu).
Mwakani patakuwa na mechi ya maveterani ya Real Madrid na Man United kwa hiyo hapo nadhani Usain atashiriki na tutamuona uwezo wake.” Alisema Ferguson.

Chanzo: Dailymail

Owen ajiunga na Stoke ila anaweza asicheze.

Michael Owen

Mchezaji Michael Owen ambaye ameachiwa huru na klabu ya Man United hatimaye ameweza pata klabu ya kumsajili ambayo ni Stoke City.
Lakini utata unakuja hapaa,Stoke walishapeleka majina 25 ya wachezaji ambao watashiriki katika kuichezea klabu hio katika msimu huu wa ligi ya Uingereza na hivyo kulazimika kuiomba Premier League ikubali kufutwa kwa mchezaji mmoja ili nafasi yake aichukue Owen.

Sheria ambazo zinaiongoza Ligi hio ya Uingereza haina sheria kama hiyo ya kutoa ruhusa ya mtu afutwe ili awekwe mwengine. Kwa hiyo majadiliano ndio yanafanyika ya aidha akubaliwe au akataliwe.

Mchezaji ambaye anatakakufutwa ni kiungo Tonge mwenye umri wa miaka 29.

Owen mwenyewe kupitia mtandao wa twitter alisema,
“Nina furaha kujiunga na Stoke, kilichobakia ni kwa Premier League wanipe ruhusa ili niweze cheza. Ninashauku ya kufanya kazi chini ya kocha Tony Pulis. Ameandaa kikosi kizuri na ninashauku wa kuanza cheza.”

Chanzo: Dailymail

Chelsea Vs Atletico Madrid 1-4 All Goals & Highlights Uefa Super Cup Final 2012

Chelsea Vs Atletico Madrid 1-4 All Goals & Highlights Uefa Super Cup Final 2012

%d bloggers like this: