Dawson na Vertonghen ndio walikuwa tofauti ya mchezo, Park ataiokoa QPR na Rooney kuichakaza Madrid


MUOKOZI: PARK JI-SUNG
Ushindi wa QPR ulipatikana kwa jitihada hasahasa za watu wawili ambao ni Jose Bosingwa na Park Ji-sung. Wote wamekuwa na mwanzo mbaya tokea wahamie QPR lakini katika mechi hii dhidi ya Sauthampton waliweza kung`aa na kuweza isaidia timu yao kuibuka na ushindi.Uzoefu wao wa kucheza katika mashindano makubwa kama Champions League ndio hasa uliowafanya waweze kung`ara.Tangu Park aihame Man UTD hii ndo mechi yake ya kwanza aliyoweza cheza katika kiwango kizuri, kiwango ambacho alikuwa akikionyesha pindi yupo United na kama akiendelea hivyo basi QPR yaweza nusurika na kushuka daraja msimu huu.

Park Ji-sung

Park Ji-sung

WALETE REAL…!!!
Rooney alifunga goli miongoni mwa magoli yaliyofungwa na United katika mechi dhidi ya Norwich na anatrajiwa kuwa mchezaji tegemeo dhidi ya Real hapo jumanne usiku. Jmabo la kufurahisha zaidi ni kuwa Welbeck alikuwa benchi katika mechi hiyo na kuleta dhana ya kuwa labda babu anataka kumtumia Welbeck kama silaha yake dhidi ya Real lakini sidhani kama ndo atakuwa mbadala wa Rooney au RVP.

Wayne Rooney

Wayne Rooney

KIJANA TOKA BRAZIL.
Philippe Coutinho ana miaka 20 tu na hana jina kubwa kama wabrazil wengine ambao wameshawahi pita au kuwika ila kijana huyu anamiguu mepesi na pia yenye kasi, aliweza wachachafya Wigan sana ingawaje sifa nyingi zimeenda kwa Suarez kutokana na hat-trick yake ila mie sifa zangu natupia kwa kijana Countinho, kwa kweli kama ataendelea hivyo na kujifunza mengine zaidi basi atakuja kuwa tishio mbeleni na kuweza iweka Liverpool mahala pazuri.

Philippe Coutinho

Philippe Coutinho

MABEKI WAWAOKOA SPURS.
Hata ukiiangalia mechi ya Arsenal na Spurs mara kumi bado utabaki na uamuzi mmoja ya kuwa beki ya Spurs ndio ilikuwa tofauti ya timu hizo mbili.Kama Michael Dawson na Jan Vertonghen wangekuwa wamevaa uzi mwekundu (jezi ya Arsenal) basi ninauhakika asilimia 120% Arsenal wangetoka na ushindi katika mechi hiyo dhidi ya watani wao wa jadi.

Michael Dawson

Michael Dawson


Jan Vertonghen

Jan Vertonghen

Advertisements

Posted on March 4, 2013, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: