Siku ya mwisho ya usajili leo.


siku ya mwisho nani aenda wapi eennh

Habari za asubuhi ndugu zangu,leo ndio siku ya mwisho ya usajili nchini Uingereza. Na mpiratz itakuletea kila litokealo nchini humo mpaka muda wa kufungwa kwa dirisha hilo. Tafadhali uwe unarefresh page yako mwenyewe kwani hakuna auto refresh, shukrani.

08:40
Inasemekana Chelsea wanataka muuza Sturridge na kumnunua mchezaji Schurrle wa Bayer Leverkusen kwa ada ya paundi mil 8.

08:43
Arsenal inasmekana inataka mchukua Essien kwa mkopo leo kabla dirisha halijafungwa.

09:10
Nigel De Jong katua Italia kwa ajili ya kujiunga na AC Milan.
“Nafurahaa kuwa hapa na AC Milan ni klabu kubwa” amesema Jong.

09:25
Charlie Adam amewasili uwanja wa mazoezi wa Stoke anafanya mazungumzo na Kocha wa Stoke Tony Pulis.
Inasemekana anahama kwa ada ya paundi mil 4 mpaka 5.

09:30
Fiorentina baada ya kumkosa Berbatov na Bendtner sasa wanafanya maongezi na Ryan Babel.

09:34
Southampton wataka msajili  Mjapan Maya Yoshida.

09:35
Mwenyekiti wa Liverpool inasemekana amepiga simu Chelsea ili kukamilisha usajili wa mkopo wa Daniel Sturridge

09:40
Taarifa: Wachezaji wote kama watahitajika cheza kesho basi lazima usajili ukamilike mchana ila ukifanyika usiku basi haruhusiwi cheza kesho.

10:19
Mdogo wa Hazard arudi nchini kwao katika klabu ya Zulte kwa mkopo akitokea Chelsea.

10:21
Van Der Vaart anasemekana yupo njiani kujiunga na Hamburg.

10:22
Breaking News: Aston Villa wametoa paundi mil 7 kwa ajili ya Dempsey na hela yao imekubaliwa mmmmh kimbebe kwa Liverpool na Sunderland maana nao pia wanamtaka.

10:23
Breaking News: Berbatov kuna uwezekano akatua Tottenham badala ya Fulham.

10:24
Danny Rose wa Tottenham anakamilisha kuhamia Sunderland kwa mkopo.

10:50
Bendtner anakamilisha usajili wake wa kutua Juventus.

10:51
Liverpool wameambiwa wanaweza msajili Damiao kwa mkopo na kisha kumsajili moja kwa moja mwisho wa msimu kwa ada ya paundi mil 13.

10:52
Afellay ajiunga na Schalke kwa mkopo akitokea Barcelona.

10:53
TAYARI: Jay Spearing wa Liverpool ajiunga na Bolton kwa mkopo.

10:54
TAYARI: De Jonga ajiunga na AC Milan

10:55
TAYARI: Kieran Richardson amejiunga na Fulham akitokea Sunderland

Richardson

14:25
TAYARI: Scott Sinclair akamilisha uhamisho wake kwenda Man City.

Sinclair

14:39
TAYARI: Charlie Adam ajiunga na Stoke City

adam

14:49
TAYARI: Danny Rose ajiunga na Sunderland kwa mkopo akitokea Tottenham.

Danny Rose

14:59
Breaking News: Tottenham wamfuatilia kiungo wa kireno Mountinho kwa ajili ya kuziba pengo la Modric.

Moutinho

15:26
Kwa wapenzi wasomaji ni ruhusa kutoa maoni yako (comments) katika blog https://mpiratz.wordpress.com/2012/08/31/siku-ya-mwisho-ya-usajili-leo-2/ au katika facebook page yetu ya https://www.facebook.com/#!/Mpiratz. sema nani wataka klabu yako imsajili katika siku ya leo ya mwisho ya usajili?

15:30
Carroll akiwasili mazoezini West Ham kwa mara ya kwanza.

Andy Carroll

15:33
TAYARI: Arsenal wamuuza Park Chu-Young kwa Celta Vigo.

15:35
TAYARI: Maicon amejiunga na Man City.

Maicon

15:39
TAYARI: Giovani dos Santos ameihama Tottenham nakujiunga na Real Mallorca kwa mkataba wa miaka minne.

16:05
Breaking News: Tottenham wamekubali kutoa paundi mil 22 kwa ajili ya kumnasa Joao Mountinho wa kutokea Porto.

16:08
Stephane Mbia yupo njiani anaenda jiunga na QPR.

16:15
Man City wajiandaa kuwasajili Javi Garcia kwa £20m na Matija Nastasic kwa £12m ukamilisho utakamilika baadae.

YAMEBAKIA MASAA 7 KUFUNGWA KWA DIRISHA LA USAJIRI

16:30
Rafael van der Vaart amekubaliana na Hamburg kuhusiana na maswala ya mshahara na sasa mchezaji huyo anajiandaa kwenda kufanya vipimo.

16:45
Inasemekana helicopter ametua Craven Cottage (uwanja wa Fulham). Je Dimitar Berbatov ndo yumo ndani??

16:47
Winga wa Valencia Hernandez yupo QPR akifanya vipimo kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

16:52
TAYARI: van der vaart amekamilisha usajili wake wa Hamburg.

Van der Vaart

16:55
Roque Santa Cruz (unamkumbuka huyo) anafanyiwa vipimo Malaga.

17:20
TAYARI:Dimitar Berbatov ni mchezaji wa Fulham sasa.

Berbatov

17:25
Liverpool wapo tayari kumuuza Henderson kwa Stoke City kwa ada ya paundi mil 8.

19:00
TAYARI:Pablo Hernandez ajiunga na Swansea kwa ada ya paundi mil 5.5

Pablo Hernandez

19:12
Breaking News: Inasemekana Michael Owen anakaribia kujiunga na Stoke.

19:15
TAYARI:Juventus wamsajili Nicklas Bendtner.

Nicklas Bendtner

19:33
Breaking News: Inasemekana Clint Dempsey amegoma kujiunga na Aston Villa na Tottenham inasemekana wapo tayari kushindana na Liverpool.

19:40
TAYARI: Gael Kakuta amejiunga na Vitesse Arnhem kwa mkopo akitokea Chelsea.

19:43
Ryan Babel amerudi Ajax baada ya kuwa mchezaji huru.

21:30
Breaking News: Daniel Sturridge yupo benchi katika mechi ya leo ya Chelsea kwa hiyo ni wazi Liverpool hawayomsajili.

21:39
Breaking News: Essien hata benchi hayupo … Mmh je swala la kwenda Arsenal laweza fanyika nini…?

21:46
TAYARI: Gaston Ramirez wa Bologna amejiunga na Southampton.

Gaston Ramirez (kushoto)

21:48
Breaking News: Fulham wameikataa ofa ya Liverpool ya kumsajili Dempsey

00:30
TAYARI: Stephane Mbia amesajiliwa na QPR kwa mkataba wa miaka miwili.

Stephane Mbia

00:31
TAYARI: Yossi Benayoun ajiunga na West Ham kwa mkopo.

00:32
TAYARI: Clint Dempsey ajiunga na Tottenham

00:33
TAYARI: Man City wamsajili Javi Garcia kwa ada ya paundi mil 15.8 akitokea Benfica.

Javi Garcia

00:34
TAYARI: Wamsajili mshambuliaji Christian Benteke kutoka klabu ya Genk kwa ada ya paundi mil 7.

00:36
TAYARI: Real Madrid wamsajili Essien kwa mkopo.

00:37
TAYARI: Everton wamemsajili Bryan Oviedo kwa mkataba wa miaka minne akitoka FC Copenhage. Paundi mil 3.5 ndio fedha zilizotumika

Bryan Oviedo

00:42
TAYARI: Stoke wamemsajili Steven Nzonzi toka Blackburn kwa ada ya paundi mil 3.5

DIRISHA LIMEFUNGWA

Advertisements

Posted on August 31, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo, Tetesi and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: