Ferguson: Tutatisha Europe nzima.


MAN.

Sir Alex amesema ya kuwa timu yake ya United itakuwa ni tishio Europe nzima baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji Robin Van Persie.

Van Persie akiwasili United

“Rooney na Robin ni wachezaji wazuri sana na itakuwa vyema sana pindi watakapo kuwa wanacheza pamoja. Itatuongezea nguvu kubwa sana mbele.
Mwaka 1999 nlikuwa na Dwight Yorke , Andy Cole, Teddy Sheringham na Ole Solskjaer ambao walitisha Europe nzima na sasa twaelekea hukohuko tena nkiwa na Javier Hernandez, Rooney, Robin, Danny Welbeck na Kagawa.
Ni mkusanyiko mzuri sana wa wachezaji na natumai ntaweza wachezesha vizuri. Ni furaha na shangwe sana kumpata mtu kama Robin kwenye timu yako” alisema Ferguson.

Emirates wakiondoa masanamu ya persie

Wenger nae alikubali ya kuwa ilikuwa ni ngumu kumbakiza Robin Arsenal,
“Ni jambo la kusikitisha kumpoteza mchezaji kama Robin, alibakiza mwaka mmoja katika mkataba wake kwa hiyo hatukuwa na njia nyingine zaidi ya kumuuza” alisema Wenger.

United wamekamilisha usajili huo mkubwa wa msimu kwa kuweza msajili Van Persie toka Arsenal kwa ada ya paundi mil 24.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: