Mourinho: Mie ni “The Only One” na sio “The Special One” tena.


Mourinho na Chelsea

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anataka kulihama jina lake la “Special One” na kuhamia “Only One”. Hii ni baada ya kocha huyo kusema anadhani anastahili jina hilo jipya kwani yeye ndiye kocha wa kwanza kuweza shinda makombe katika ligi zote tatu bora barani Ulaya.

Mourinho na Inter Milan

Kocha huyo mwenye asili ya Kireno ameweza shinda ligi ya Hispania na timu yake ya Real Madrid ambako imemuongezea sifa za kushinda makombe ya ligi yakiwemo la Italia mara mbili alipokuwa na Inter Milan na Uingereza mara mbili pindi alipokuwa na Chelsea na pia kombe la ligi ya Ureno mara mbili pindi alipokuwa na Porto na bila kusahau kushinda Champions League mara mbili.

Mourinho na Madrid

“Nimepende au hata usiponipenda mimi ni wakipekee, nimeweza shinda mataji katika ligi tatu kubwa barani Ulaya. Kwa hiyo nadhani badala ya kuniita “Special One” watu waanze niita “Only One”.
Baada ya kushinda takriban kila kitu nimekuwa sasa nataka wale wa karibu yangu nao pia kupata faraja.
Mwaka 2010 nlichaguliwa kuwa kocha bora duniani na mwaka 2011 nlikuwa wa pili lakini sasa sijali nipo nafasi ya ngapi.
Nakaribia timiza miaka 50 na najihisi ndo kwaanza kama naianza upya ukocha.” alisema Mourinho.

Mourinho “The Only One”

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 15, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: