Agger: Sitaki kuondoka.


Agger

Mchezaji wa Liverpool Daniel Agger ameiambia klabu yake ya Liverpool kuwa hataki kuondoka na hataki imuuze ingawaje pamekuwa na tetesi kuwa Man City wanamtaka.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Denmark, tayari zilishakuja ofa mbili toka Kwa Man City kwa ajili ya kumsajili lakini Liverpool imezikataa ofa zote huku Barcelona nao wakiwa njia kutaka kumsajili mchezaji huyo.

Akiwa anaongea na Gazeti la Nchini kwao Agger alisema mpaka sasa hajaambiwa kuhusiana na chochote kuhusu Man City na kuwa hatopenda enda huko.
“Sijaambiwa chochote na klabu yangu kuhusu uhamisho. Sio juu yangu kufanya uamuzi huo, kama klabu ndio imeamua hivyo mie siwezi fanya lolote.
Kipindi hiki cha usajili kila mwaka kimekuwa na tetesi, lakini mie sisemi neno. Mpaka sasa sijaambiwa chochote kwahiyo sioni sababu ya mie kuwa na wasiwasi. Nimeskia tu pembeni kuwa Man City wananitaka lakini sijajua mpaka sasa Liverpool wanalionaje hilo.
Mimi ninafuraha na mahala nilipo sema klabu yatakiwa jua ni kipi yakitaka. Kwa upande wangu ni bora nibakie Liverpool.
Liverpool wanaweza niuza ingawaje nimebakiza miaka miwili katika mkataba na wala sijabadilisha mawazo ya kuwa nisingependa chezea klabu nyingine hapa Uingereza zaidi ya Liverpool.
Sio vyema kukaa mahala usipohitajika lakini kwangu bora nibakie Liverpool, hilo ndio pendekezo la moyo wangu.

YNWA

Agger ambaye yupo na timu yake ya taifa akijiandaa na mechi ya kirafiki wiki iliyopita alidhihirisha mapenzi yake kwa Liverpool kwa kujichora Tatoo katika vidole vyake ya YNWA, YNWA ikisimama badala ya maneno YOU’LL NEVER WALK ALONE maneno hayo ndio kauli mbiu ya klabu hiyo ya Liverpool.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 15, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: