Mchezaji wa Italia ajifunga minyororo akigomea adhabu.


Emanuele Pesoli

Mchezaji wa zamani wa timu ya Siena Emanuele Pesoli amejifunga minyororo katika geti la Chama cha mpira cha Italia kwa nia ya kupinga adhabu ambayo amepewa jana ya kufungiwa kucheza kwa takribani miaka mitatu.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anachezea timu ya Hella Verona iliyopo daraja la pili nchini Italia alipewa adhabu hiyo na chama cha soka cha nchini humo (FIGC) baada ya kugundulika ya kuwa alihusika katika upangaji matokeo (mechi).

Adhabu hiyo aliipata baada ya wachezaji wenzake wa zamani Carlo Gervasoni na Filippo Carobbio kusema ya kuwa mchezaji huyo (Pesoli) alihusika katika upangaji wa matokeo katika mechi ya Siena dhidi ya Varese mwezi wa tano mwaka 2011.

“Ntakaa hapa mpaka mwisho wangu unikute.
Namsubiri Raisi wa FIGC Giancarlo Abete.
Wananiharibia maisha yangu kwa jambo ambalo sijalifanya, ntalipinga swala hili kwa kila namna niwezavyo.
Nimeumia sana kwa adhabu hii na pia nataka nikutane na hao wananisingizia.” alisema Pesoli.

Pesoli anaruhusiwa kukataa rufaa mpaka ifikapo Agosti 20 na pia anataka kukutana na Carobbio na Gervasoni uso kwa uso ili auseme ukweli.
Sakata hili la upangaji matokeo pia limemkumba kocha wa Juventus Antonio Conte ambaye amefungiwa kwa mda wa miezi 10.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on August 12, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: