Mexico 2 Brazil 1 (Olympic).


Mexico

Wakuvaa moja hawezi vaa mbili kamwe, huu msemo leo umewapata tena Brazil baada ya kufunga katika fainali ya mashindano ya Olympic na timu ya Mexico. Brazil ambao hawajawahi shinda medali ya dhahabu katika mashindano hayo ya Olympic walikuwa wanatarajia kuondoa gundu hilo leo lakini kwa bahati mbaya historia bado ikawa inawaandama na matokeo yake wakachezea kichapo.

Mexico wakishangilia

Oribe Peralta akifunga la kwanza

Ni mchezaji Oribe Peralta ndie aliyefunga magoli yote mawili kwa Mexico na kuweza ipatia nchi yake ubingwa huo wa Olympic huku goli la brazil likifungwa na Hulk.

Oribe Peralta akifunga la pili

Oribe Peralta

Mexico walianza mashindano haya wakiwa wanafikiriwa kama wasindikizaji tu na Brazil wakipewa kipaumbele cha kutwaa ubingwa lakini leo hii mbele ya umati wa watu 86,162 Mexico wameweza onyesha ya kuwa hao ni moto wa kuotea mbali.

Neymar majonzini

Kuanzia safu ya ulinzi, viungo mpaka ya mashambulizi Brazil leo ilikuwa butu huku Mexico wa kiwa kinyume chake. Sio Neymar, Marcelo, Oscar, Damiao wala Pato wote walikuwa ni majoka ya kibisa leo mbele ya wanamexico.

Mashabiki wa Mexico

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 11, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: