Mancini: United ndio watakuwa mabingwa.


Roberto Mancini

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amesema timu ya Manchester United ndio inapewa kipaumbele cha kushinda ligi na huku akisema timu yake ya City itashika nafasi ya tatu au hata ya nne.

Van Persie

Mancini amesema hayo baada ya kuchukizwa na swala la klabu yake kutoweza sajili wachezaji ambao amekuwa akiwataka kama Van Persie wa Arsenal, Daniel Agger wa Liverpool, Daniele De Rossi wa Roma na Eden Hazard ambaye sasa amejiunga na Chelsea.

Akiwa anajiandaa na mechi ya jumapili dhidi ya Chelsea, Mancini amesema Chelsea wamejijenga vyema baada ya kushinda Champions League kwa kuwasajili Hazard, Marko Marin na Oscar.

“United wanaanza wakiwa na asilimia kubwa ya kutwaa kombe, Sie labda tutakuwa wapili ,watatu au hata wanne.
Unaposhinda taji ni vyema ukaimarisha kikosi chako lakini sio uimarishe siku kumi (10) kabla dirisha la usajili halijafunga bali uufanye usajili huo miezi miwili kabla.

Kwa sasa ni ngumu kununu mchezaji kwasababu unaponunua mchezaji timu iliyouza inakuwa haina muda wa kutosha wa kununua mchezaji wa kuziba pengo la aliyeondoka. Kwa hiyo zinapobakia siku 20 inakiwaga vigumu sana kufanya usajili.” alisema Mancini.

Chanzo: ESPN

Advertisements

Posted on August 11, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: