Tottenham wamtenga Modric.


Luka Modric akifanya mazoezi peke yake

Kiungo wa timu ya Tottenham Luka Modric ametengwa na timu hiyo na mpaka kufikia hatua ya kuambiwa afanye mazoezi peke yake. Mchezaji huyo anajiandaa na msimu mpya akiwa anafanya mazoezi peke yake huku uhamisho wake wa kwenda Real Madrid ukiwa bado haueleweki.

Uamuzi wa kumtenganisha Modric na wachezaji wengine ni dalili tosha ya kuwa meneja Villas-Boas anajiandaa na maisha ya Tottenham bila ya Modric. Hii sio mara ya kwanza kwa kocha huyo kufanya hivyo kwani alishawahi kufanya swala kama hilo kwa Anelka na Alex pindi alipokuwa Chelsea baada ya wachezaji hao kuonesha nia ya kutaka kuondoka.

Modric

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amekataa ofa ya Madrid ya paundi mil 30 kwa kukusudia kama kweli Madrid wanamtaka basi watoe paundi mil 40. Maongezi kati ya klabu hizo yanaendelea huku Madrid wakigoma kutoa kiasi hicho cha fedha.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 10, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: