Rooney kurudi Everton.


Rooney milele na everton

Wayne Rooney ametabiriwa kuja kumalizia mpira wake akiwa ndani ya jezi ya Everton, utabiri huo umefanywa na mkongwe wa Everton Tony Hibbert.

Tony Hibbert ameichezea klabu hiyo ya Everton kwa takribani mika 16 sasa na leo siku ya jumatano katika mechi ya Everton dhidi ya AEK Athens ndio itakuwa mechi ya kumpongeza veterani huyo.

Beki huyo ambaye amecheza mechi 309 tokea aanze chezea Everton mwaka 2001 alimtaka Rooney aje ashiriki katika mechi hiyo ya kumpongeza lakini kwa bahati mbaya United nao pia leo wana mechi.

Hibbert

Ingependeza kama Rooney angekuwepo na akacheza, imekuwa bahati mbaya tu kwamba United nao pia wanamechi leo.
Nlipomuambia aliudhika sana baada ya kugundua kuwa Man United pia wanamechi maana alitaka sana kuja katika mechi hii ya kunipongeza. Bado naongea na Rooney na ninafurahishwa kumuona akipata mafanikio.
Tokea nkipo mjua mpaka sasa hajabadilika hata kidogo kuhusiana na mapenzi yake kwa mpira.
Najua kuja kwake angepata mapokezi mabaya lakini ukweli ambao wote twaujua ni kuwa Rooney bado ni mwanaevertoni mpaka moyoni”.

“Najua anaweza fanya chochote kwa Everton na ilikuwa ni faraja kwangu alipokubali kuja kucheza mechi yangu sema ndo hivyo tena United nao wana mechi pia.
Natarajia kuwa Rooney atakuja malizia mpira wake hapa Everton na klabu itakuwa yakijinga sana ikimkataa mchezaji kama Rooney.” Alisema Hibbert.

Wayne Rooney na Tony Hibbert

Hibbert ambaye amezaliwa Huyton ambayo ni wilaya moja na Steven Gerrard wa Liverpool, kila anachokifanya Hibbert ni kwa manufaa ya Everton na hata kocha wake David Moyes ashawahi thubutu sema Hibbert damu yake ni ya blue na milele atakuwa na nafasi katika klabu hiyo.

Chanzo: Dailymail 

Advertisements

Posted on August 8, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: