Liverpool waambiwa Allen atawagharimu.


Joe Allen

Kocha wa timu ya Swansea Michael laudrup amewatahadharisha liverpool ya kuwa mchezaji wake Joe Allen hawatompata kwa bei rahisi.

Swala la mchezaji huyo kuihama Swansea na kwenda jiunga na Bosi wake wa zamani katika klabu ya Liverpool limekuwa likiongelewa kwa mda mrefu sasa na huku ikisemekana Swansea walishakataa ofa ya mwanzo ya Liverpool ya paund mil 12.5 kwa ajili ya Allen.

Katika mkataba wa Allen kuna kifungu ambacho kinamruhusu kuuzwa kwa paund mil 15, hivyo Laudrup atasimamia hapohapo kwani anajua Liverpool wanauwezo wakutoa kiasi hicho kama walivyoweza awali kwa jordan henderson na stewart Downing.

Laudrup

Nimchezaji bora na hivyo bei yake ni kubwa.
Kocha wa Liverpool anamjua vyema Allen na kama anataka kuwabadilisha Liverpool basi anamuhitaji mchezaji kama Allen katika kiungo.
Tumewaona wakinunua viungo kwa bei ya juu hapo awali lakini kiukweli Allen anauwezo zaidi yao na hivyo bei yake itakuwa kubwa“. Alisema kocha wa Swansea Laudrup.

Pia yasemekana kocha huyo alikataa ofa ya kuwa Liverpool watoe fedha pamoja na kuwapa Jonjo Shelvey kwa mkopo, akidai ya kuwa hawezi pokea mchezaji kwa mkopo toka Liverpool kama mchezaji huyo sio wa first eleven.
Alipoulizwa kuhusiana na swala hilo Laudrup alijibu ya kuwa,

Kama watatupa Suarez labdaa… Tunawachezaji wazuri hapa na hao pia wanawachezaji wazuri lakini sijaona mcheza wa Liverpool ambaye hayupo First eleven anayeweza kuja kwetu eti akawa katika First eleven yetu, hapo bado sijaona. Wanataka fanya hivyo ili walipe fedha kidogo tu hawana sababu nyingine.”

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on August 7, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: