Rodgers: Liverpool twamtaka Dempsey.


Clint Dempsey

Kocha wa Liverpool,Brendan Rodgers amesema Liverpool wanafanya mikakati ya kumsajili Clint Dempsey na pia akaongeza ya kuwa Andy Carroll ahatoruhusiwa kuondoka kwa mkopo.

Brendan Rodgers.

Rodgers ambaye yupo na timu yake Boston Marekani ameonesha dhamira hiyo ya kumsajili Dempsey ambaye amebakiza miezi 12 katika mkataba wake na Fulham. Fulham wanataka paundi mil 10 kwa ajili ya mchezaji huyo.

“Clint ni mchezaji ambaye tumekuwa tukimtaka.
Ian Ayre mkurugenzu wetu anafanya maongezi na Fulham ili kuangalia nini cha kufanya. Clint ni mchezaji mzuri sana lakini hatutaki ongea mengi” Alisema Rodgers.

Andy Carroll

Kuja kwa Dempsey maanake  nafasi za Carroll kubakia Liverpool zinazidi kuwa finyu na Rodgers hakusita kuliongelea hilo.

“Kumtoa kwa mkopo mtu ambaye klabu ililipa paundi mil 35 kwake hilo halitowezekana.
Andy atachukuliwa kama wachezaji wengine, kama kuna ofa itatolewa tutaiangalia na kutoa uamuzi”.

“Naskia watu wanasema ya kuwa hawezi fiti katika staili yangu ya uchezaji. Lakini kama ulinunuliwa kwa paundi mil 35 basi nina uhakika unaweza fiti na kucheza staili ya aina yoyote ile.
Carroll ni mchezaji mzuri na atajiunga na wenzake wiki ijayo”. Alisema Rodgers.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 19, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: