Suarez aazisha varangati la Evra tena.


Suarez and Evra

Luis Suarez ameanzisha varangati la swala lake na Evra tena ingawaje aliambiwa na klabu yake ya Liverpool kuwa asiliongelee swala hilo tena.

Suarez

Mchezaji huyo toka Uruguay amesema Man United walitumia mabavu yao yakisiasa ambako ikapelekea yeye kufungiwa mechi nane (8) msimu uliopita.

Mchezaji huyo alisema aliudhiwa sana na swala la hilo ambako akishia kutokwa hadi na machozi.

Akoingea na TV ya nchini kwao, ambako wanajiandaa na mashindano ya Olympic. Suarez alilianzisha upya swala hilo la ubaguzi..

Katika maongezi hayo Suarez alisema ya kuwa mabosi wake wa Liverpool wamemkataza kulizungumzia swala hilo la Evra tena lakini yeye hajaskia na kuamua kupasua jipu upyaaa.

chanzo

“Ilikuwa ni ngumu kuvumilia mambo yaliotokea.
Huwa sionyeshagi hisia zangu nkiwa uwanjani lakini nje ya uwanja huwa naonyesha na kusema ukweli nililia sana kuhusiana na swala lile la Evra”.

“Wiki ambayo nilikuwa naenda mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi ilikuwa ni wiki ngumu sana maishani mwangu. Mke wangu na mie tulilia sana ndani ya wiki ile.
Watu ndani ya Liverpool waliamini ya kuwa ni mbinu ambayo Man United waliitumia ili tu kuipoteza Liverpool katika ramani na pia kunichanganya mimi kimpira.
Lakini ndani ya Uingereza Man United ina nguvu kubwa sana kisiasa, kwa hiyo inakulazimu ujinyamazie tuu”. Alisema Suarez.

Pia akaendelea kwa kusema ya kuwa hakuwa na mpango wakukataa kusalimiana na Evra ila Evra ndiye aliyesababisha yote hayo yakatokea.

“kila mtu (yeye na Evra) alimuelewa mwenzake vibaya tu katika swala la kusalimiana.
Kwanza nadhani lile swala lilipangwa ili mie nionekane mbaya, kwani mwishowe ni mie tu ndio nliyeadhibiwa”.

“Nilimuahidi mke wangu, Meneja wangu na wakurugenzi kuwa ningeshikana mkono na Evra.
Niliadhibiwa kwasababu yake lakini sikuwa na kinyongo nae.
Katika vyombo vya habari vya Uingereza kilichoonekana ni kipindi mie nlipompita lakini hawajaonesha mwanzo kabisa ambako nlipotaka mpa mkono wangu yeye aliushusha wa kwake.
Vyombo vya habari vya Uruguay na vya Hispania tu ndio vilionesha ukweli halisi uliotokea.”

“Ilkuwa inanibidi nipande taxi kwenda Manchester kwa ajili ya kusikiliza kesi. Nilikuwa naamka saa moja asubuhi na kurudi nyumbani  saa 3 usiku. Nilikuwa nachoka sana. Nilitamani kulia na kuvunjavunja kila kitu vya pembeni yangu lakini nilikuwa ninashindwa kwa sababu mtoto wangu alikuwepo nyumbani. Zilikuwa ni siku mbaya sana maishani mwangu ila nashukuru mashabiki wa Man United wananiheshimu”.

“Siku moja baada ya sakata hilo la kukataa kushikana mikono na Evra, nilikuwa katika mgahawa nakula chakula cha mchana na mke wangu. Mara akaja shabiki wa Man United na akaniomba apige picha na mie na akaniambia nakuhusudu sana”.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on July 18, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: