Liverpool wawakatali kuwapa Newcastle Andy Carroll…


ANDY CARROLL

Newcastle walidhihirisha nia yao ya kumsajili Carroll kwa kupeleka maombi rasmi kwa Liverpool ya kumchukua Andy Carroll kwa mkopo lakini maombi hayo yalikataliwa.

Liverpool ambao walimnunua Carroll kwa ada ya paundi mil 35 toka kwa Newcastle miezi 18 iliyopita.

mashabiki wa Newcastle wakimzomea Carroll

Kocha wa Newcastle Alan Pardew alitoa sifa nyingi za kumpamba mchezaji huyo wiki iliyopita na akasema angependa sana kuwa nae klabuni kwake.

mashabiki wa Newcastle wakimzomea Carroll

Carroll mwenyewe hataki kuondoka Liverpool na yupo tayari kugombania namba yake na kijana mpya aliyetua hapo Liverpool Fabio Borini.

Kocha wa Liverpool alipouluzwa kuhusu swala la Andy Carroll aligoma kutoa jibu la kueleweka kama mchezaji huyo atabakia au ataondoka.
“Hana tofauti na wachezaji wengine ambao wapo hapa Liverpool.
Wanaweza wakawa na kila kitu lakini akili yao ikawa haipo kimchezo.
Sio vyema kumsema Carroll kuwa yupo tofauti kwani Andy ni kijana mzuri sana, kwa hiyo tutaangalia mipango yetu itakuwaje na nini chakufanya” alisema Rodgers.

likizo

Liverpool wanaenda Marekani kwenye mechi zao za majaribio lakini Andy hatokuwepo. Yeye pamoja na wenzake walioshiriki Euro 2012 wote bado wapo likizo.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: