Kete ya kwanza Simba leo kwa URA


MABINGWA mara sita wa Kombe la Kagame Afrika Mashariki na Kati, Simba inaanza kampeni zake leo itakapopambana na URA ya Uganda katika mchezo wa tatu wa michuano ya hiyo iliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa.

Simba ambayo ilitwaa Kombe la Urafiki Alhamisi iliyopita kwa kuilaza Azam FC penalti 3-1 baada ya sare ya 2-2, itaingia uwanjani ikiwa na kikosi kilichokamilika wakiwemo wachezaji kadhaa wapya.

Kocha wa Simba, Cirkovik Milovan aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa wachezaji wake wameimarika, isipokuwa bado anapambana na safu ya ushambuliaji ambayo bado haijatulia.

“Nina wachezaji wazuri na naamini wanaweza kufanya maajabu…lakini bado safu ya ushambuliaji haijatulia sana, lakini nimejitahidi kutengeneza mfumo wa timu utakaoiwezesha kupachika mabao kirahisi.”

Kocha huyo ametengeneza mifumo kadhaa ambayo hata hivyo hubadilika kulingana na mchezo unavyokwenda. Simba hutumia mfumo wa 4:2:4 na wakati mwingine 5:3:2 na 4:4:2.

Katika mechi yao na Azam, Simba ilitumia mfumo wa 4:2:4 ambayo viungo wawili walikuwa wakishuka kusaidia kuokoa na kuacha wawili mbele na kutengeneza mfumo mwingine wa 4:4:2

Naye kocha wa URA, Alex Isabirye alisema kuwa wamekuja kwenye michuano ya Cecafa wakiwa na matumaini ya kurudi Uganda wakitabasamu wakiwa na kombe kwa mara ya kwanza.

Timu hiyo iliyopoteza fainali mbili, 2007 ilifungwa na APR mabao 2-1 ikiwa chini ya kocha, Frank ‘Video’ Anyau mjini Kigali, Rwanda na mwaka 2008 ilikuwa chini ya Moses Basena, ikachapwa na Tusker ya Kenya idadi hiyo mjini Nairobi.

Mara ya mwisho ilishiriki michuano hiyo mwaka 2010 chini ya Isabirye na ilimaliza nafasi ya mwisho kwa kufungwa na Sofapaka 3-0, Atraco ya Rwanda 4-0 kabla ya kuilaza Simba 2-1.

Isabirye atakuwa na kibarua cha kujenga jina Cecafa licha ya timu yake kuwa na matatizo katika lango, ngome na ushambuliaji kazi aliyokuwa anairekebisha Isabirye kabla ya kuja Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, URA haina historia pana katika ukanda wake ikiwemo kutwaa ubingwa japokuwa ina heshima yake kwa kuwa ni kati ya timu tishio za michuano hiyo.

Wakati huohuo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetupa pingamizi lililowekwa na Simba la kumzuia mchezaji Kelvin Yondani aliyesajiliwa na Yanga ili asicheza michuano ya Kombe la Kagame.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema usajili wa Yondani kwenda Yanga toka klabu ya Simba hauna utata hivyo ameruhusiwa kushiriki mashindano hayo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on July 15, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: