Samata moto TP Mazembe


Mbwana Samata (mbele)

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na TP Mazembe, Mbwana Samata anaongoza kwa kupachika mabao 13 katika klabu hiyo kwa sasa.

Samata alifikisha idadi hiyo baada ya kufunga mabao mawili na kuiongoza TP Mazembe kuisambaratisha Muungano kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya DR Congo iliyofanyika kwenye Uwanja mpya wa Mazembe kwa mara ya kwanza mjini Lubumbashi.

Mbali ya Samata wengine waliofunga kwenye mchezo huo ni viungo wa Zambia, Rainford Kalaba, Nathan Sinkala na Luka Lungu.

Kocha wa TP Mazembe, Lamine Ndiaye alilazimika kumuanzisha Samata katika mechi hiyo baada ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kulalamikia uamuzi wake wa kumuanzisha benchi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Katika mechi hiyo TP Mazembe ilichapwa mabao 2-1 na Al Ahly huku bao lao likifungwa na Samata aliyeingia akitokea benchi.

Kocha Ndiaye alisema hakumuanzisha Samata katika mechi hiyo kwa sababu alikuwa akisumbuliwa na tumbo muda mfupi kabla ya mechi dhidi ya Al Ahly.

Mchezaji anayemfuatia Samata kwa kufunga mabao mengi katika klabu ya TP Mazembe ni Luka Lungu aliyefunga mabao 12 mpaka sasa katika mashindano tofauti.

TP Mazembe hivi sasa inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 34.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on July 14, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: