Furaha kwa Man United baada ya Vidic kurudi…


Nemanja Vidic …

Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic amewapa matumaini Man United kwa kurudi tena mazoezini baada ya kuwa na nje kwa majeruhi kwa mda mrefu.

Nemanja Vidic

Msebia huyo aliungana mazoezini na mchezaji mpya wa Man United Shinji Kagawa pamoja na wengine ambao hawakucheza katika mashindano ya Euro 2012.

Vidic aliumia goti katika mechi ya Champions League dhidi ya FC Basel na kuweza kumfanya akose mechi zote zilizokuwa zimebakia msimu mzima.

Kurudi kwake ni shangwe kwa Man United na Ferguson kwa maana kutawasaidia kuimarisha beki yao vyema na kuweza kupigania ubingwa wa ligi dhidi mahasimu wao Man City.

Shinji Kagawa ..

Mjapani Kagawa ambaye alisajiliwa kutokea Borussia Dortmund kwa paundi mil 17 nae pia alikuwa mazoezini na wachezaji wenzake.

Berbatov ambaye anasemekana anataka kuondoka nae alikuwepo mazoezini, huku timu za Malaga na PSG wakiwa wanamfuatilia kwa karibu ili kuweza msajili mchezaji huyo.

United watasafiri wikiendi hii kuelekea Afrika ya kusini ambako watacheza na timu ya Amazulu FC ya jijini Durban siku ya Jumatano na kisha watacheza na Ajax Cape Town siku ya Jumamosi.

Chanzo: Dailymail 

Advertisements

Posted on July 14, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: