Drogba apokelewa kwa Shangwe na kudai Uchina kafuata mpira na sio pesa..!!


karibu shenghai

Didier Drogba amesema kilichomfanya ahamie Uchina ni kutokana na sababu za kimpira na sio kifedha.

mashabiki wakimlaki Drogba

Takribani mashabiki 300 walikusanyika kwa ajili ya kumpokea mchezaji huyo pindi alipowasili kwa ajili ya kujiunga na timu yake ya Shanghai Shenhua.

mashabiki wakimlaki Drogba

Drogba amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na klabu hiyo ya Uchina na kumpelekea kupokea mshahara wa paundi 270,000 kwa wiki.

nimekuja kimpira

“Nimeamua kujiunga na klabu hii kutokana na sababu za kimpira.
Pindi klabu hii iliponifuata ilinieleza mikakati yake na nikaona ni dhahiri wanania ya kukuza soka la China.
Ilikuwa rahisi kwangu kujiunga na timu nyingine za Ulaya lakini nkaamua kuja hapa kwani naamini China ni sehemu yenye kupenda michezo”.Alisema Drogba

Drogba alifanikiwa kufunga magoli 157 katika mechi 341 ambazo alichezea Chelsea na kumfanya kuwa namba nne katika orodha ya wafungaki bora wa Chelsea.

mashabiki wakimkaribisha Drogba

Drogba atajiunga na mchezaji mwenzake Anelka ambaye nae pia yupo klabuni hapo. Klabu hiyo ipo katika nafasi ya 13 katika ligi hiyo ya China ambayo ina jumla ya klabu 16 zinazoshiriki ligi hiyo, huku kocha wa zamani wa Argentina Sergio Batista akiwa ndio kocha wa timu hiyo.

“Matokeo ya klabu yangu sio mazuri.
Lakini n’gwe ya pili ya msimu imeenza kwa hiyo itabidi tujitahidi ili kuipeleka timu katika nafasi nzuri
Mie na wenzangu tutajitahidi kucheza kadri ya uwezo wetu.
Nimekuja hapa kucheza na kushinda mataji na sio kwa ajili kustaafu”. Alisema Drogba

mashabiki wakimkaribisha Drogba

Alfajiri na mapema mashabiki waliwasili Shanghai Pudong International Airport kwa ajili ya kumkaribisha mchezaji wao mpya.

Drogbaaaaaaaaaa….

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 14, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: