Arsenal waomba Mungu kuwa Van Persie afanye kama Rooney…


Van Persie

Arsenal wanaelekea wiki ya mwisho ya majidiliano na mchezaji wao Van Persie na wakitarajia mchezaji huyo atabadilisha mawazo yake na kusaini mkataba mpya kama alivyofanyaga Rooney kwa Man United.

Nahodha huyo wa Arsenal aliwashangaza na kuwashtua wengi pindi aliposema mipango ya klabu hiyo haipo sawa na kuwa hayupo tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

maongezi yahitajika

Van Persie anatarajiwa kurudi wiki ijayo mazoezini na hapo kocha wake Wenger atajaribu kuongea nae kwa ukaribu zaidi na labda ataweza mfanya mchezaji huyo kubadilisha mawazo yake.
Huku viongozi wengine wa Arsenal wakiamini ya kuwa usemi alioutoa Van Persie mwanzo ulitolewa na msemaji wake ili tu aweze pata mshahara mkubwa zaidi kama ilivyokuwa kwa Rooney mwaka 2010.

Wayne Rooney alitishia kuondoka kumbe kisa pesa

Mpaka sasa Van Persie ameahidiwa mkataba wa miaka mitatu ambao utamfanya awe anapokea paundi mil 130,000 kwa wiki pamoja na bonas ya paundi mil 5.

Kama mkataba mpya usiposainiwa basi itabidi Wenger amuuze mchezaji huyo kabla mkataba wake haujaisha kabisa na matokeo yake akampoteza kwa bure.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 14, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: