Terry ashinda kesi..


Terry akitoka mahakamani kifua mbele.

John Terry ameshinda kesi ambayo alikuwa akituhumiwa kumtusi na kumbagua beki wa QPR Anton Ferdinand.

chanzo

Pindi hukumu ilipotolewa na Hakimu Howard Riddle ya kuwa Terry hana makosa, Shangwe na furaha ilimjaa Terry ambaye alitikisa kichwa kwa furaha.
Kisha akaruhusiwa kuondoka mahakamani hapo na hakutaka kusema kitu chochote. Alipelekwa moja kwa moja mpaka katika gari amabalo lilikuwa linamsubiri.

Terry akitoka mahakamani kifua mbele

Nje ya mahakama Mwanasheria wa Terry alisema,
Mahakama leo imeamua kutupilia mbali mashtaka yote yaliokuwa yameelekezwa kwa John Terry. Terry ameweza jieleza vyema kwa FA, polisi na mahakama.
Hakumtukana Mr.Ferdinand na mahakama imeweza ona hilo.
John anawashukuru wanasheria wake wote waliomsaidia kushinda kesi hii, rafiki zake na klabu yake ya Chelsea”.

Hakimu alitoa hukumu yake ya mwisho kwa kusema,
Kesi ilikuwa inahusu ubaguzi uliosemekana umefanywa na Mr Terry.
Ameweza toa ushahidi wa kutosha ya kuwa ya kuwa yeye sio mbaguzi“.

mashabiki

Wakati anaingia mahakamani Terry alipata maneno ya kumtia nguvu toka kwa mashabiki wake walikuwepo nje ya mahakama. Familia za pande zote mbili zilikuwepo kusikiliza hukumu ambayo ingetolewa.
Baada ya hakimu kutoa hukumu yake klabu ya Chelsea haikuchelewa kutoa shukrani zao kwa mahakama hiyo kwa kusema,
Chelsea Football Club inashukuru na kuheshimu hukumu ya hakimu Howard  Riddle ya kufuta kesi ambayo ilikuwa inamkabili J.Terry, tunashukuru na kuamini ya kuwa itamsaidia mchezaji wetu kuweza kuhamisha akili yake kwenye mpira na kuweza isaidia timu yake ambayo ipo kwenye hatua za maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya“.

mahakamani

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: