Mbelgija amtema Nsajigwa Kagame


kocha Tom Saintfiet

SIKU za nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kuendelea kuichezea klabu hiyo zimeanza kuhesabika baada ya jana kuenguliwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 wa kocha Tom Saintfiet kitakachoshiriki Michuano ya Kagame.

Uamuzi huo wa Saintfiet ni pigo jingine kwa Nsajigwa ambaye hivi karibuni aliliripotia kutaka kuachwa na mabingwa hao kutokana na kushuka kiwango, pia alidai kuhusika katika kusababisha Yanga kufunga 5-0 na Simba mwishoni mwa msimu uliopita.

Akizungumza na Wanahabari kocha  Saintfiet alisema hakumjuisha Nsajigwa kwenye kikosi hicho kwa lengo la kumpatia muda wa kutosha wa kupumzika na awe tayari kwa kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu hapo baadaye.

“Nsajigwa ni mchezaji mzuri, lakini nimeamua kumpumzisha kwenye michuano hii kwa sababu msimu uliopita alicheza mechi nyingi na sasa anahitaji kumpumzika ili awe tayari kwa Ligi Kuu.

“Sababu nyingine iliyonifanya nichukue uamuzi huu ni kwamba katika nafasi yake kuna wachezaji wengi vijana walioonyesha soka ya kiwango cha juu, hivyo nataka kuwapa uzoefu wa kutosha wa mechi za kimataifa,” alisema Saintfiet.

Wachezaji wapewa nafasi ya kurithi namba ya Nsajigwa kwenye michuano ya Kagame ni David Luhende, Juma Abdul, Oscar Joshua, na Godfrey Taifa.

Nahodha huyo wa Yanga alianza kupata pigo msimu huu baada ya kuumia mwezi Oktoba 2011 na kushindwa kuichezea Taifa Stars katika mchezo wake dhidi ya Morocco wa kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2012. Pia, alivuliwa unahodha wake kwenye kikosi cha Stars kinachonolewa na kocha Kim Poulsen.

Mbali ya Nsajigwa wachezaji wengi wa Yanga walioachwa na kocha Saintfiet ni pamoja na majeruhi Nurdin Bakari na kiungo chipukizi Frank Domayo, Simon Msuva na Omega Seme wanatumia timu ya taifa ya Vijana iinayojiandaa na mechi za kimataifa dhidi ya Rwanda na Nigeria.

Pamoja na kuwakosa nyota hao bado Mbelgiji Tom anaamini anakikosa bora zaidi cha kutetea ubingwa wake wakiongozwa na Nadir Haroub, Haruna Niyonzima na Nizar Khalfan.

Wakati huo huo; Mshambuliaji wa Polisi ya Rwanda, Meddy Kagere amekiri  kufanya mazungumzo na Yanga, lakini bado hajaamua kusaini mkataba nao.

“Nimezungumza na viongozi wa Yanga, walikuwapo nchini Jumatano (juzi), lakini bado sijakubaliana nao,”alisema Kagere.

“Klabu yangu ya Polisi imeniambia inanitaka, tutakaa chini na kuzungumza, sidhani kama itawezekana mimi kuichezea Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame kama inavyotangazwa,”alisema Kagere ambaye ni mchezaji muhimu wa timu ya Polisi ya Rwanda.

Kauli ya Kagere inatarajiwa kumfurahisha rais wa klabu ya Polisi, Alphonse Katarebe ambaye anaamini kwamba klabu yao inatakiwa kuwalinda wachezaji wake nyota ili kupata mafanikio.

Kama Yanga ikifanikiwa kumsajili Kagere atakuwa ni mchezaji wa pili kutoka Rwanda kuichezea klabu hiyo baada ya Haruna Niyonzima.

Kikosi cha Yanga: Makipa Yaw Berko  na Ally Mustapha.
Mabeki ni David Luhende, Juma Abdul, Oscar Joshua, Godfrey Taifa, Kevin Yondani, Ladislaus Mbogo na Nadir Haroub.
Viungo ni Stephan Mwasika, Athuman Idd ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’ na Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Idrisa Rashid.
Washambuliaji  Hamis Kiiza, Said Bahanuzi, Jerryson Tegete, na Shamte Ally.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: