Maxi Rodriguez aihama Liverpool…


Maxi Rodriguez

Liverpool imetangaza ya kuwa mchezaji wao Maxi ameondoka klabuni hapo na kurudi nchini kwake Argentina  kujiunga na klabu yake ya zamani ya Newell’s Old Boys.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitua Liverpool akitokea Atletico Madrid Januari 2010 na kuweza fanikiwa kufunga magoli 17 katika mechi 73 alizochezea timu ya Liverpool.

Kocha mpya wa Liverpool Rodgers alijaribu mshawishi mchezaji huyo kubakia lakini jitihada hizo zimegonga ukuta, baada ya Maxi kuamua kurudi katika klabu yake ya zamani alioacha miaka 10 iliyopita.

Website ya Liverpool imesema ya kuwa,
Liverpool FC amethibitisha ya kuwa Maxi amejiunga na Newell’s Old Boys ya Argenrtina.
Kila mtu kutoka Liverpool FC kwapamoja twapenda tumshukuru Maxi kwa msaada wake alioutoa na twamtakia kila lililo la kheri mbeleni“.

Maxi nae aliwaandikia barua mashabiki wa Liverpool isemayo,
Dear Reds, Mie Naondoka Liverpool FC leo.

Kabla sijajiunga na LFC, nlikuwa naijua ni klabu tu ambayo ni kubwa Ulimwenguni katika maswala ya mpira kama klabu nyinginezo. Lakini baada ya kuhamia hapa nimegundua kuwa hii sio klabu kubwa tuu ila ni Familia kubwa na nzuri.

Nimejaribu kucheza kwa uwezo wangu wote pindi nlipokuwa naivaa jezi ya Liverpool. Imekuwa ni faraja kwangu kuweza kuivaa na kuitetea jezi hii ya LFC kwa mda wote huu wa miaka miwili na nusu. Ninarudi nyumbani na sunduku ambalo limejaa kumbukumbu nyingi nzuri kuhusu hapa, marafiki wazuri nliowapata na pia Familia nzima ya LFC.

Nashukuru sana kwa msaada na ukarimu wenu. Ni vigumu kueleza ni kiasi gani faraja nliyokuwa naipata pindi The Kop walipoimba jina langu katika wimbo,… ‘Maxi, Maxi Rodriguez runs down the wing for me da da da dada…’

Hasta la vista“.

Maxi.

Chanzo: Skysports.

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: