Liverpool wakubaliwa paundi mil 12 kwa ajili ya Fabio Borini.


Fabio Borini

Mchezaji huyo wa kiitalia ndo atakuwa usajili wa kwanza wa Rodgers tangia ametua Liverpool.

Liverpool wamekubaliana na Roma kutoa paundi mil 12 kwa ajili ya kumpata mchezaji Fabio Borini amabako usajili huo unatarajiwa kukamilika wikiendi hii.

Borini anasemekana kama ni mchezaji nyota anayechipukia hii ni baada ya kufanya vizuri katika klabu yake ya Roma na kupelekea hata kupata nafasi katika kikosi cha Italia cha Euro 2012.

Rodgers anamjua Fabio vizuri kwani alimfundisha akiwa nae Chelsea, pia alimchukua kwa mkopo akiwa Swansea ambako aliwasaidia sana kuweza kuwafanya wapande daraja na kuingia ligi kuu.

Borini ameweza funga goli katika kila mechi mbili na kuweza kumpatia nafasi katika timu ya Taifa iliyoshiriki Euro 2012.

Parma na Roma ndio klabu zilizommiliki mchezaji huyo lakini mwishowe Roma walimnunua toka kwa Parma kwa ada ya paundi mil 6 na sasa Liverpool wametoa mara mbili yake ili kuweza mpata mchezaji huyo.

Kutua kwa Borini kunaweza kuwa ndio mwisho wa Andy Carroll na kupelekea uvumi ya kuwa Carroll anaweza tolewa kwa mkopo kwenda Milan, huku West Ham nao wakimtaka.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: