Liverpool wakamilisha usajili wa Borini..


Fabio Borini atua Liverpool

Liverpool wametangaza ya kuwa Fabio Borini amejiunga na klabu hiyo baada ya kufanya vipimo vya afya na kisha kusaini mkataba na klabu hiyo.

Fabio Borini atua Liverpool..

Mchezaji huyo mwenye asili ya Italia amefanya vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wake huo mpya na Liverpool.

Kutua kwake Liverpool kumemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Brendan Rodgers.
Borini na Rodgers wanafahamiana vizuri kwani wameshafanya kazi pamoja wakati wakiwa Chelsea, Swansea na sasa safari yao yaendelea wakiwa Liverpool.

vipimo

Uwezo wa Borini wa kucheza na nyavu umeweza mfanya mpaka akachaguliwa katika kikosi cha taifa cha Italia amabacho kilishiriki katika mashindano ya Euro.

Liverpool inafuraha kutangaza ya kuwa imemsajili mchezaji wa AS Roma Fabio Borini.
Mchezaji huyo wa Italia amesaini mkataba wa muda mrefu na klabu hii baada ya kufanikiwa kupita vipimo vya afya.
Kujiunga kwake na Liverpool kunamfanya awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Brendan Rodgers” ilisema taarifa toka kwenye website ya Liverpool.

Borini atavaa jezi namba 29 kwani ndo namba aliyoiomba apewe na kusema ya kuwa ndio namba ya bahati kwake.

Nataka kufunga magoli na kuweza ifikisha Liverpool Champions League na kuisadia Liverpool kwa kila namna .
Sina kikubwa cha kusema ila, kupitia kwa Brendan Liverpool itacheza mpira tena mpira wa kuvutia“. Alisema Borini.

Chanzo: Skysports

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: