Kolo Toure kwenda Bursaspor kwa paundi mil 6.


Kolo Toure

Bosi wa timu hiyo ya Uturuki Ertugrul Saglam amesema ya kuwa klabu yake ipo katika maongezi na nahodha wa zamani wa Arsenal na inatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo.

Mchezaji huyo wa Man City, Kolo Toure anataka kusajiliwa na klabu ya Bursaspor ya Uturuki, hii ni kutokana na Toure kushindwa kusaini mkataba mpya na Man City kuhofia kutopewa nafasi za kucheza za kutosha.

Toure amesema atafurahi kama atapata timu itakayomuwezesha cheza kila siku hata kama ni nje ya Uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitua Man City baada ya kununuliwa na Mark Hughes kwa ada ya paundi mil 16 na sasa anataka kuuzwa kwenda Uturuki kwa ada ya paundi mil 6 tu.

“Tumekuwa katika maongezi na Kolo Toure kwa takribani siku mbili sasa.
Itakuwa ni furaha sana kwetu kama akitua klabuni hapa.
Tunajitahidi kadri ya uwezo wetu ili usajili huu uweze fanyika”. Alisema Ertugrul Saglam.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on July 13, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: