Madega ataka uchaguzi wa amani


SIKU chache kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo wa viongozi wa Yanga,aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Imani Madega amewataka wanachama wa klabu hiyo kufanya uchaguzi kwa amani na kuchagua viongozi watakaoleta mapinduzi ya kweli ndani ya klabu hiyo.

Uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ili kupata Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.

Akizungumza na Mwananchi, Madega alisema ni wakati wa wanachama wa Yanga kujitambua na kufahamu wajibu wao katika kupata viongozi wenye uchungu na klabu yao pamoja na kuhakikisha wanawapigia kura watu ambao watabadirisha taswira ya timu yao na kuleta maendeleo ya kweli.

Alisema akiwa bado ni mwanachama hai wa klabu hiyo anapenda kutoa wito kwa wanachama wenzake kutumia fursa ya kupiga kura kwa amani na utulivu huku akiwataka watambue kuwa wapo katika kipindi ambacho timu yao inahitaji umakini mkubwa wa kutetea kombe la mashindano ya Kagame ambayo yatakuwa tayari yameanza.

“Kikubwa mimi napenda tu kuwaasa wanachama wenzangu kutumia uchaguzi huu kupata viongozi ambao wanaona watawafaa na watakuwa chachu ya maendeleo kwa klabu yao, pia wapige kura kwa amani huku wakitambua kuwa timu yao ipo katika kazi kubwa ya kutetea ubingwa wa Kagame na wachezaji wanahitaji utulivu na umakini mkubwa,”alisema Madega.

Akizungumzia mashindano ya Kagame yatakayoanza Jumamosi, Madega alisema ana matumaini makubwa na mabingwa watetezi Yanga kutokana na maandalizi yao huku akiwatakia mafanikio mema ya kuhakikisha wanatetea ubingwa wao kwa mara nyingine.

Watakaowania nafasi katika uchaguzi wa Yanga ni John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhan kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti waliopita ni Ayoub Nyenzi, Clement Sanga na Yono Kevela.

Wajumbe waliopita ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Kampira, Mohamed Mbaraka ‘Binkleb’, Ramadhan Said, Edgar Fongo, Ahmed Gao, Beda Tindwa, Jumanne Mwamenywa na George Manyama.

Wengine ni Gadeuncius Ishengoma, Haron Nyanda, Omary Ndula, Shaban Katwila, Justine Baruti, Jamal Kisongo, Peter Haule.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on July 12, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: