Fergie: Narudi tena sokoni baada ya Kagawa na Powell.


Bunduki mpya za Fergie

Sir Alex Ferguson amefurahishwa na usajili alioufanya mpaka sasa lakini amesema kuna uwezekano mkubwa akarudi tena sokoni kusajili mchezaji mmoja wa mwisho.

Akiongea katika chumba cha mahojiano na waandishi wa habari, Fergie alisema ni kazi ngumu sana kufanya usajili kama kuna mashindano makubwa yanafanyika kama ya Euro.

Lakini anataka kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya na kuhakikisha kikosi chake kipo imara na tayari kwa ajili ya kupambana na Man City katika kugombania ubingwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa kusajili wachezaji wengine labda mmoja au hata wawili hivi kabla ya kuanza kwa msimu”
Panapokuwa na mashindano makubwa kufanya usajili inakuwa ni ngumu sana. Lakini sasa Euro imeisha tutajaribu kusajili wachezaji zaidi.
Tumekuwa tukijitahidi kupata wachezaji kabla kumalizika kwa kipindi cha usajili”.

Kwa swala la Kagawa palikuwa na maongezi ya mda mrefu sana lakini kwa Powell ilikuwa rahisi kwasababu twamjua Mwenyekiti wa mpira wa klabu ya Crewe (Dario Gradi) kwa hiyo ilikuwa ni rahisi kwetu”.

Nilimuuliza Dario kama Nick anaweza cheza kama kiungo. Dario akasema anadhani anaweza na Nick pia anasema anaweza. Kwa hiyo twategemea kumtumia kama kiungo na kumkuza kama kiungo.
Kagawa yeye atacheza mbele zaidi ya Powell. Hatutakiwi kusema mchezaji mmoja atabadilisha timu ila ninaimani ataongeza nguvu ya ziada.
Kama akiendelea funga magoli kama alivyokuwa akifunga basi itakuwa safi sana“. Alisema Fergie.

Chanzo: Skysports

Advertisements

Posted on July 12, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: