ANFIELD KUOGOPEKA TENA..


ANFIELD

Ni takribani zaidi ya miaka mitatu sasa imepita na Timu ya Liverpool haijawezashiriki mashindano ya Champions League. Ni zaidi ya miaka mitatu sasa haijawepo katika nafasi za nne bora za ligi na ni takribani miaka mitatu sasa uwanja wa ANFIELD umekuwa shamba la bibi kwa timu zingine kuja kujichukulia pointi.

Rodgers..

Brendan Rodgers (mzee wa Tik Tak) ndio kocha mpya wa Liverpool, ndio aliyechaguliwa kurudisha heshima ya Liverpool, ndiye alichaguliwa kuirudisha Liverpool Champions League ,ndiye mwenye mpango wa kuifanya Anfield kuwa tishio kwa wapinzani wajapo uwanjani hapo.

Rodgers katua Liverpool na falsafa yake ya mpira wa chini, mpira wa pasi, mpira wa kasi na mpira wa kushambulia.
Staili hiyo ilianzia kwa Liverpool ya miaka ya 70-80.
Liverpool ya akina Kevin Keegan, Kenny Dalglish mpaka kwa Ian Rush.
Ikahamia kwa Liverpool ya miaka ya 90. Liverpool ilioshehena viungo imara kama akina Redknapp na John Barnes, Mawinga hatari  akina Steve Mcmanaman na Washambuliaji wenye kujua nyavu kama akina Collymoore,Fowler,Michael Owen na Heskey.
Liverpool hii ilishehena wachezaji kama akina Mcateer beki mwenye spidi ya Glenn Johson, ukabaji wa Martin Kelly na nguvu za Jose Enrique. John Barnes kiungo aliyekuwa na Ukabaji wa Lucas Leiva na upigaji pasi wa Gerrard. Steven Macmanuman aliyekuwa na Speedi mithili ya Downing na Bellamy chenga za Suarez na Uharaka wa Raheem Sterling na Suso.

Liverpool inarudi tena kwa wachezaji wenye sifa mithili ya wa miaka ya kuanzia 70 mpaka 90.
Rodgers anapenda mpira wa chini, anapenda mpira wa pasi ,anapenda mpira wa aina ya Tik Tak.
Tik Tak ni mpira wenye asili ya Hispania ambao mpaka leo Barcelona ndio staili wanaoitumia.
Tit tak ni staili ambayo anaifanya timu kuweza kumiliki mpira kwa muda mrefu na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kuweza kufunga magoli.
“Tunapokuwa na mpira kila mchezaji ni lazima acheze. Tofauti yetu na timu nyingine ni pindi tunapokuwa na mpira tunacheza na wachezaji 11 wote hali yakuwa timu nyingine zacheza na wachezaji 10 na kipa” alisema Rodgers.
Tik Tak inaweza tumika katika Staili ya 4-4-2, 4-3-3 au hata 4-5-1.

Tik Tak

Mstari wa 1: KIPA MCHEZAJI (The Sweeper goalkeeper)

Sehemu hii ni sehemu ya chini kabisa ya staili ya Tik Tak ambayo inacheza sehemu kubwa kuliko sehemu zingine ya staili hii. Kipa anahitajika kutumia miguu sana na kuhakikisha anapiga pasi za uhakika. Kipa anapaswa kuwa makini kwa mipira ya juu na ya chini, awe mjasiri,asiwe na uoga na awe mwenye kuenjoy kuuchezea mpira. Kipa huyu anatakiwa apokee mipira/ kurudishiwa mipira pindi timu yake inaposhambuliwa ili kuwapunguzia presha wachezaji wa ndani. REINA anavigezo vyote hapo.

Mstari wa 2: MABEKI (The Libero)

mabeki

Wachezaji hawa wanakuwa kama Kipa ,kwani kazi yao ni kuondoka na kupunguza presha wazipatazo Viungo. Mabeki hawa mmoja anatakiwa awe mwenye kutumia akili sana na mwengine awe na nguvu na uwezo wa kupigana vikumbo.Mabeki hawa wanakuwa na uwezo wa kuona yote yanayotokea mbele na hivyo kuweza kuwaelekeza wa mbele ni wapi na ni nini cha kufanya.AGGER na SKRTEL wanfaa sana hapa.

Mstari wa 3: KIUNGO MCHEZESHAJI. (The Volante de salida)

Lucas Leiva

Mchezaji huyo anatakiwa kuwa na uwezo wa kukaa sana na mpira na pia kuupata pindi anapopokonywa. Awe na uwezo wa kuusoma mchezo na daima akipata mpira anatakiwa atoe pasi na kuwa tayari kuupokea haraka iwezekanavyo.kwa Barca hapa ni Xavi.
“Napokea pasi, natoa pasi, napokea, natoa tena”. (Xavier 2011).
Kwa Liverpool hapa Gerrard,  Lucas Leiva pamoja na Spearing ndio wanafaa nafasi hii.

Mstari wa 4: MAWINGA (The Wing backs)

GLENN JOHNSON

Wachezaji hawa wanatakiwa kuwa tayari kukimbia juu mpaka chini kila dakika kwa ajili ya mashambulizi na ukabaji. Upigaji wa krosi hautopigwa katika chaki ila wanapaswa kuingia nao mpira mpaka ndani na hapo ndio kama krosi basi waipigie wakiwa ndani.
GLENN JOHNSON,MARTIN KELLY na JOSE ENRIQUE,ROBINSON ndio wanao weza cheza nafasi hizo.

Mstari wa 5: KIUNGO KAMILI (The box to box creative Midfielders)

Steven Gerrard

wachezaji hawa wanatakiwa kuwa na uwezo wa kubadilisha mchezo mda wowote na pia wanatakiwa kutafuta nafasi ilikuweza pokea mpira kila dakika na kuwa na uwezo wa kutoa pasi za mwisho.JONJO SHELVEY, CHARLIE ADAM, GERRARD,AQUILANI na HENDERSON wanauwezo wa kucheza hapo.

Mstari wa 6: WASHAMBULIAJI WA NDANI (The Inside Forwards)

Luis Suarez

Niwachezaji wanaotakiwa kuwa na spidi, akili na uwezo mkubwa wa kuchezea mpira na upigaji chenga. Wachezaji hawa wanatakiwa kuwapa tabu mabeki kwa uwezo wao walionao wa kuwatesa mabeki. LUIS SUAREZ, BELLAMY,MAXI, JOE COLE,RAHEEM STERLING,SUSO na PACHECO wanauwezo wakucheza nafasi hizo kwa Liverpool.

Mstari wa 7: MSHAMBULIAJI. (The Linking target man)

Carroll..

Mchezaji huyo anatakiwa kuwa nauwezo mkubwa sana akiwa na mpira pia na hata asipokuwa na mpira.Awe na uwezo mkubwa wa kuungana na wachezaji nyuma yake.CARROLL anaweza kufaa nafasi hii lakini kama MAXI au mchezaji wa AS Roma FABIO BORINI anayesemekana anatua Liverpool ndio atafaa zaidi.

Mstari wa 8: SEHEMU YA KUFUNGA (The goal-scoring opportunity and assist zone)

Sehemu hii ni sehemu muhimu kwa kila mchezaji atakayeingia hapa kwa kuhakikisha ni lazima afanye kila awezalo ili goli lipatikani aidha kwa kufunga mwenyewe au kutoa pasi ya uhakika ya goli.

BR

Hiyo ndio Tik Tak staili ya Rodgers, staili mpya ya Liverpool, Staili mpya ya Anfield.
“Nataka timu zikiwa zinakuja Anfield ziwe zinakuja na uoga wa kufungwa na sio ujasiri wa kuondoka na ponti” alisema Rodgers.
Liverpool ilikuwa na kupata umaarufu kupitia SHANKLY na mbeleni kumpata Mfalme wao KING KENNY  na sasa ni Rodgers time,the time of the Tik tak way.

LFC

Advertisements

Posted on July 10, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Shuti la leo and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: