Park Ji-Sung atua QPR..


Park Ji-sung

Park amejiunga na klabu ya QPR kwa mkataba wa miaka miwili.
Mkorea huyo mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na klabu hiyo kwa bei ambayo haijafahamika bado.

Park Ji-sung akitambulishwa

Park ni Usajili wa sita kwa timu ya Mark Hughes ambako tayari ameshawasajili Ryan Nelsen, Andy Johnson, Rob Green, Samba Diakite na Fabio wa Man United.

Park Ji-sung…

QPR walinusurika kushuka daraja msimu uliopita na hawataki kosa hilo lijirudue kwa kuhakikisha wanafanya usajili wa nguvu.

Park ambaye alikuwa akiichezea Man United amejiunga na QPR tayari akiwa ameshawahi kutwaa mataji ya Ligi ya Uingereza mara nne (4) na Champions League mwaka 2008.
Pindi alipokuwa Man United alifanikiwa kucheza mechi 203 na kufunga magoli 27.

enzi

Kocha wa QPR Mark Hughes hakusita nae kugawa sifa kwa mchezaji.
“Katika sekta ya mpira Ji ni mchezaji ambaye nimekuwa nikimkubali sana uwezo wake akiwa uwanjani.
Ameivaa jezi ya Man United kwa kujituma mpaka mwisho na natumai atafanya hivyohivyo hapa pia.
Nilisema mwisho wa msimu uliopita ya kuwa hatutaki kuwa katika hali ya kugombania kushuka daraja tena na ninaamini tupo katika hali nzuri sasa.” alisema Mark Hughes.

Park ambaye amejiunga na QPR akitokea Man United nae alisema,
“Najua QPR wanataka kuimarisha timu yao na mie naahidi kujitahidi kila niwezalo kuisaidia timu hii.
Kulikuwa na ofa nyingine nyingi lakini hii ya QPR ilikuwa ni ya kipekee”

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on July 9, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: