Tanzania yapanda kwa nafasi 12 Fifa


TANZANIA imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) vilivyotolewa jana na hivi sasa inashika nafasi ya 127.

Kwa mujibu wa viwango vya Fifa, mwezi uliopita Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 139,sasa imepanda baada ya kufikisha pointi 253 tofauti na mwezi uliopita ilikuwa na pointi 214.

Tanzania imepanda baada ya mwezi uliopita kucheza na Ivory Coast na kufungwa mabao 2-0, pia ilicheza na Gambia na kushinda 2-1 kabla haijatoka sare ya 1-1 na Msumbiji.

Mechi kati ya Tanzania dhidi ya Msumbiji ilikuwa ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 na mechi dhidi ya Ivory Coast pamoja na mechi dhidi ya Gambia zilikuwa ni mechi za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2014.

Matokeo ya sare iliyopata Tanzania ilipocheza dhidi ya Msumbiji mjini Maputo, yalisababisha kupigwa penalti na hivyo Tanzania kutolewa katika mashindano ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2013.

Katika kufuzu Fainali za Kombe la Dunia hivi sasa Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa imezidiwa na Ivory Coast ikizitangulia Morocco na Gambia.

Uganda imeendelea kuongoza Ukanda wa Afrika Mashariki katika nafasi ya 85 ikipanda nafasi tisa ikifuatiwa na Kenya  nafasi ya 125 kisha Rwanda nafasi ya 126.

Nchi ya Burundi katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki yenyewe inashika nafasi ya 136.

Huu ni mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) ambapo ameanza kazi na kuipandisha Tanzania katika viwango hivyo vya Fifa.

Viwango hivi vya Fifa ni muhimu katika upangaji wa ratiba za mechi, ambapo nchi zinazoshika nafasi ya juu hupewa nafasi mbili za juu katika kila kundi la timu nne na zile zinazoshika nafasi za chini hupewa nafasi mbili za chini.

Kutokana na Tanzania kuwa katika nafasi za chini katika viwango hivi vya Fifa imejikuta kila mara ikipangiwa timu ngumu kwenye mashindano na hivyo kutolewa katika hatua za awali.
Ivory Coast inashika nafasi ya 16 katika viwango vya Fifa na kuendelea kuongoza kwa upande wa Afrika, ambapo pia ilikuwa katika nafasi hiyohiyo kwa viwango mwezi uliopita.

Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia, ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa ubora wakishika nafasi ya kwanza.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on July 5, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: