Galatasaray wamtaka Berba..


Berbatov

Timu ya Galatasaray imedhihirisha nia yake ya kutaka kumnunua mchezaji wa Man utd Dimitar Berbatov.

Berbatov amesema ya kuwa anataka kuondoka Man Utd katika kipindi hiki cha kiangazi baada ya kucheza mechi tano tu za ligi katika msimu ulioisha.

Timu yake ya zamani ya Bayer Leverkusen imejitoa katika mbio za kumnyakua mchezaji huyo, huku kukiwa na tetesi pia za kuwepo na uwezekano wa mchezaji huyo kutua PSG.

Lakini Uturuki ndio mahala panaonesha mchezaji huyo ndipo anaweza kwenda baada ya Raisi wa Galatasaray Unal Aysal Kutangaza dhahiri nia ya klabu yake kutaka kumnunua mchezaji huyo.

“Mbulgaria huyu ni mchezaji mzuri sana. Nataka ajiunge nasi lakini uamuzi wa mwisho ni wa kocha Fatih Terim kuamua” alisema Aysal.

Berbatov amefunga magoli 57 katika mechi 149 alizoichezea Man Utd.

Chanzo: Skysports 

Advertisements

Posted on July 3, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: