Okwi kufanya majaribio Italia


Emmanuel Okwi

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi anataraji kwenda kufanya majaribio nchini Italia mapema mwezi ujao.

Safari ya Okwi itaanzia nchini Uganda hapo Julai 4 na uongozi wa Simba ukisisitiza taratibu zote za safari yake zimekamilika.

Akizungumza na jijini jana, Afisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema mchezaji huyo ataenda Italia akitokea Uganda moja kwa moja. .

“Okwi tutamkosa katika Kagame kwa sababu atasafiri Julai 4 kuelekea Italia  kufanya majaribio na endapo atafuzu basi ataingia nayo mkataba  moja kwa moja,” alisema Kamwaga.

Katika hatua nyinyine Simba itavaana na Mafunzo ya Zanzibar keshokutwa katika mashindano ya Kombe la Urafiki yaliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katika mashindano hayo Tanzania bara itawakilishwa na klabu za Simba,Yanga na Azam yanalenga kudumisha muungano na umoja.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on June 30, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: