Giovani dos Santos aondoka Tottenham na kuhamia La Liga..


Giovani Dos Santos

Kiungo huyo wa Tottenham ambaye amesahaulika kabisa anatarajia kuihama klabu hiyo na kurudi nchini Hispania aidha klabu ya Sevilla au Atletico Madrid ambazo zote zinamtaka mchezaji huyo mwenye asili ya Mexico.

Mchezaji huyo ambaye ana umri wa miaka 23 amepewa ruhusa ya kuondoka katika kambi ya Timu ya taifa kwa ajili ya kuweza kufanikisha maswala yake ya kuhama White Hart lane.

Dos Santos alijiunga na Spurs akitokea Barcelona mwaka 2008 kwa ada ya paundi mill 6 na ada ya paundi mill 5 itarajiwa kutolewa kulingana na mechi atakazo cheza. Lakini mpaka sasa amefanikiwa kucheza mechi mbili tu za Spurs.

Kocha wa timu ya Mexico Luis Fernando Tena alisema,” Aliniomba ruhusa ili aweze kukamilisha maswala yake ya uhamisho kutoka Tottenham kwenda klabu nyingine. Inamlazimu kusaini makaratasi.
Kitu cha muhimu ni utulivu wa akili, kama kuhama kwake klabu ndio swala zuri kwake basi ni bora alifanye, alituambia jina la klabu lakni hatuwezi sema ni klabu gani”.

Chanzo: Guardian

Advertisements

Posted on June 30, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: