Yavunja mkataba wa Asamoah, alamba Sh20mil


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah amevuna Sh20 milioni kutokana na Yanga kuvunja mkataba wake jana.

Asamoah ni miongoni mwa wachezaji 10 waliotangazwa kuachwa na Yanga msimu huu kutokana na kushindwa kuonyesha cheche msimu uliopita katika mechi mbalimbali za kirafiki na mashindano.

Awali uongozi wa Yanga ulishindwa kuvunja mkataba wa Asamoah baada ya mchezaji huyo kutaka alipwe Sh30 mil pamoja na mshahara wa mwaka mmoja kwa ujumla wake vilikuwa Sh42milioni.

Baada ya mazungumzo kati ya uongozi na mchezaji huyo raia wa Ghana, amekubali kulipwa Sh20mil na mshahara wa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa mtoa habari amedai Asamoah huenda akalipwa fedha zaidi mwanzoni mwa wiki ijayo na kuruhusiwa kurejea kwao.

Msimu uliopita, Asamoah ndiye aliyekuwa kinara wa ufungaji kwa Yanga kwa kufunga mabao 10 katika Ligi Kuu pamoja na bao lake la kichwa lililowezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame waliposhinda 1-0 dhidi ya mahasimu wao Simba mwaka jana.

Mbali ya Asamoah, wengine walioachwa ni Davis Mwape wa Zambia, Idd Mbaga, Julius Mrope, Kigi Makasi, Atif Amour, Godfrey Bonny, Abuu na Zuberi Ubwa na Bakari Mbegu, huku kipa Shabaan Kado akitolewa kwa mkopo Mtibwa Sugar.

Wakati huo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Fredy Felix Minziro  amesema anakunwa vilivyo na muungano wa washambuliaji wake wapya, Said Bahanuzi na Saimon Msuva na kudai kuwa ujio wao katika klabu yake utakuwa wa tija.

Akizungumza jana baada ya pambano la kirafiki kati ya Yanga na Kijitonyama United, Minziro alisema licha ya ugeni wao, nyota hao wameonyesha uelewano mkubwa kiasi cha kuifanya safu yake ya ushambuliaji iwe kali zaidi katika kupachika mabao.

“Kwa ujumla maandalizi yetu yanaendelea vizuri na zaidi nikwambie tu kwamba napata amani zaidi baada ya kuona washambuliaji wapya wanafanya kazi vizuri.

“Kama uliangalia mpira uliona jinsi Msuva na Said Bahanuzi wanavyoelewana vizuri ni dalili nzuri kwamba tutakuwa na safu makini zaidi  hasa ukizingatia kuna wazoefu ambao wanasaidiana nao kama Jerry Tegete ,”alisema Minziro na kuongeza:

“Hata muungano wa Nizar Khalfan na Juma Seif na Chuji ni nzuri nitawaangalia zaidi Jumamosi tutakapocheza na Express, lakini nina uhakika hadi kufikia Kombe la Kagame tutakuwa tumeiva vyakutosha.”

Yanga jana iliizabua Kijitonyama United mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki ya timu hizo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Bora.

Mabao ya Yanga katika mechi hiyo yalipachikwa na Juma Abdul, Said Bahanuzi, Omega Seme na Athuman Iddi ‘Chuji’.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on June 29, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: