Balotelli: Kwa ajili yako Mama..


Balotelli akimkumbatia mamaake (Silvia) na kumzawadia magoli jana baada ya mechi dhidi ya Ujerumani.

Mario Balotelli ameivukisha Italia kwenda katika Fainali ya Euro 2012 na kisha akasema magoli aliyoyafunga yote ni zawadi kwa mama yake.

Mchezaji huyo wa Man City alielekea katika majukwaa baada ya Mechi ya jana ambako ndipo alipokuwepo mama yake na kumkumbatia kisha akamuahidi kuwafunga na Hispani.

“Nimepata nini toka mchezo wa leo..?, baada ya mechi nimeenda alipokuwepo mama na nkamwambia Magoli nliyoyafunga ni zawadi yako.
Usiku huu ni usiku mzuri sana kwangu, lakini natarajia Jumapili itakuwa zaidi. Kilichobaki ni kupumzika na kuwafunga Hispania Jumapili.
Sisi na Hispania ndio timu bora katika mashindano haya. Je twaweza shinda..?? Ntakujulisha jibu lake Jumapili”alisema Balotelli

Mario Balotelli

Balotelli akaendelea kwa kusema ya kuwa magoli yote yalikuwa “RAHISI” na kuwashukuru wachezaji wenzake.

“Goli la kwanza lilitokana na pasi nzuri ya Cassano. Cassano akikutumia pasi basi ufungaji huwa ni rahisi.
La pili lilitokana na pasi nzuri toka kwa Montolivo. Kwa kawaida nafungiaga kona ya mbali ila hili niliamua fungua kona ya karibu” alisema Balotelli

kocha wa Italia alimsifia Balotelli kwa kusema kuwa Balotelli ni “Unique”.

Prandelli alisema,”Balotelli mpira ulimkubali, alikuwa yupo makini na alitekeleza nlichomuagiza. Ni mchezaji mwenye uwezo sana.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on June 29, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: