Juve watoa £14.5 na mchezaji ili kumpata Suarez..


Suarez

Habari toka Tottosport zasema ya kuwa Juventus wanajiandaa kutoa fedha kwa ajili ya kumnyakuwa mchezaji wa Liverpool Luis Suarez. Inasemekana wanataka toa Paundi mill 14.5 pamoja na mchezaji Milos Krasic ili waweze pewa Suarez.

Itakuwa ngumu kwa Liverpool kuikubali ofa hiyo kutoka kwa Juve ambao ndio mabingwa wa ligi ya Italia huku magoli yao mengi yakifungwa na viungo na sio washambuliaji na ndio maana wanamuhitaji Suarez ili kuweza rekebisha tatizo hilo.

Milos Krasic amekuwa akifuatiliwa na Liverpool kwa mda mrefu sasa na hata kocha mpya wa Liverpool inasemekana anamtaka lakini swala la kumjumuisha mchezaji huyo kama mjumuisho wa fedha ili Juve wampate Suarez ni jambo ambalo Krasic na Rodgers kamwe hawatolikubali.

Suarez alimaliza msimu uliopita akiwa na magoli 17 na pasi za goli/mwisho 11. Kiufupi ni kwamba Kwa Liverpool Suarez ni lulu amabayo kuipoteza itakuwa ni majuto.

Chanzo:Caughtoffside

Advertisements

Posted on June 24, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: