Shabiki wa Liverpool afungiwa kwa kumtusi Evra..


Phillip Gannon

Shabiki wa timu ya Liverpool amefungiwa kuhudhuria kuangalia mpira kwa mda wa miaka minne baada ya kugundulika ya kuwa amewatusi mashabiki wa Man Utd na kumbagua nahodha wao Patrice Evra.

Shabiki huyo Phillip Ganon mwenye umri wa miaka 58 alionekana kupitia Live Television akifanya vitendo vya ubaguzi na huku akiigiza kuwa kama nyani.iliambiwa mahakama ya Liverpool ambayo ndo yaendesha kesi hiyo.

Vitendo hivyo vilitokea katika uwanja wa Anfield Januari 28 ya mwaka huu katika mechi ya FA raundi ya nne.

Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana tangia kufungiwa kwa Suarez kwa kosa la ubaguzi wa rangi dhidi ya Evra.

Katika dakika ya 23 ya mchezo kamera za TV zilimnasa shabiki huyo wa liverpool akivifanya vitendo hivyo vya ubaguzi. Baadae habari zilisambaa kupitia mtandao matokeo yake mambo yakafika mpaka mahakani.

Gannon ambaye ni fundi seremala alipatikana na makosa zaidi akiwa ndani ya mahakama kwa kutumia maneno mabaya ndani ya mahakam hiyo.

Luis Suarez na Patrice Evra

Makosa yote hayo yamejumuishwa na kutolewa hukumu ya kuwa Gannon amefungiwa kuhudhuria mechi za Liverpool na za Uingereza kwa mda wa miaka minne na pia hatoruhusiwa kwenda mjini kama Liverpool itakuwa inacheza. Pia alipigwa faini ya paundi 180.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 23, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: