Michelsen kuzinoa timu za taifa za vijana


MRITHI wa aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya vijana, Kim Poulsen amewasili nchini juzi kwa ajili ya kuzinoa timu za vijana chini ya miaka 17 na 20.

Kocha huyo Jakob Michelsen raia wa Denmark ameanza kibarua chake na jana alikuwa mjini hapa kusaka vipaji vya vijana katika mashindano ya shule za sekondari ngazi ya taifa (Umisseta) yanayoendelea kwenye viwanja vya Shirika la Elimu.

Kocha huyo aliambatana na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwa ajili ya kuangalia vipaji vya vijana ambao wataitwa katika timu hizo za vijana.

“Kocha huyu amewasili juzi na hivi sasa tumeanza mikakati ya kuangalia vipaji ili kupata wachezaji wa timu za vijana,” alisema Julio na kuongeza kuwa watakuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha wanaibua vipaji katika mashindano ya Umisseta.

Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni alithibitisha ujio wa kocha huyo na kufafanua kwamba ndiye atakayechukua mikoba ya Kim.

Kayuni aliliambia gazeti hili wilayani hapa kwamba Michelsen atashirikiana na Julio katika kusimamia timu hizo za vijana.

“Michelsen na Julio tuko nao hapa Kibaha lengo likiwa kutafuta vipaji vya vijana na ndiyo wamepewa mikoba ya kuzinoa timu hizo,” alisema Kayuni.

Kim alipandishwa kufundisha timu ya wakubwa ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikinolewa na Jan Poulsen ambaye amemaliza mkataba wake na kurudi kwao Denmark.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on June 23, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: