Mchakato wa Uchaguzi TFF kuanza Julai 1


KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, imetangaza tarehe ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi kwa wanachama na muda wa ukomo wa kukaa madarakani utakwisha kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa mchakato wa uchaguzi kwa vyama hivyo utaanza Julai 1 na kumalizika Novemba 10.

“Kwa mujibu wa katiba ya TFF ibara ya 49 (1) vyama wanachama wa TFF ambavyo muda wao wa ukomo wa madaraka utamalizika Desemba 2012 na mchakato wa uchaguzi utaanza Julai 1,” alisema Wambura.

Wambura alisema kuwa vyama vya wilaya  ambavyo muda wa ukomo wa madaraka ya uongozi umekwishapita na havijafanya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni havitaruhusiwa kushiriki chaguzi za vyama vya mikoa.

“Kuna vyama vya wilaya  ambavyo muda wa ukomo wa madaraka ya uongozi umekwishapita na havijafanya mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa kanuni, hivi vielewe kwamba vimepoteza sifa ya kushiriki chaguzi za vyama vya mikoa.

Wanachama wengine wa TFF ni pamoja na vyama vya soka vya wilaya na klabu za Ligi Kuu.

Wakati huo huo, Mkutano wa dharura wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) utafanyika Juni 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy, ajenda kuu katika mkutano huo ni marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayotokana na maelekezo ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya marekebisho kwenye katiba za wanachama wake ambazo zina upungufu.

Tayari mapendekezo ya marekebisho hayo kulingana na mwongozo wa TFF yalishapitiwa na Kamati ya Utendaji ya TWFA.

Mbali ya Kamati ya Utendaji, wajumbe wengine wa mkutano huo ni Mwenyekiti, Katibu na mjumbe wa Mkutano Mkuu kutokana vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.

Chanzo: Mwananchi.

Advertisements

Posted on June 22, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: