Madrid watoa paundi mil 30 kwa ajili ya Modric..


Modric.

Klabu ya Real Madrid ya Hispania inajiandaa kutoa paundi millioni 30 kwa ajili ya kumpata kiungo wa Tottenham Luka Modric. Hii ni baada ya kocha Jose Mourinho kuimbia klabu yake itoe ofa kwa ajili ya kumpata mchezaji huyo.

Madrid wanapewa asilimia kubwa ya kumpata mchezaji huyo kuliko Man Utd ambao wamekuwa wakivumishwa kumtaka mchezaji huyo kila kukicha lakini mpaka leo hakuna cha maana kilichofanyika ili kuweza kumpata mchezaji huyo.

Uhamisho wa kiungo huyo anayechezea Crotia utampatia kocha mpya wa Tottenham fedha za kuweza kusajili wachezaji zaidi.

Bye bye Tottenham..??

Modric anataka kuondoka Tottenham na kwenda katika Klabu ambayo inacheza mashindano ya Champions League. Lakini Tottenham hawataki kumuuza mchezaji huyo ingawaje ofa kubwa ikija itakuwa ngumu kuikataa.

Mpaka sasa Tottenham hawana kocha na wamejaribu kuongea na makocha wengi ili kuweza jaza nafasi hiyo wakiwemo AVB na Laurent Blanc ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Lakini kitendo cha Mwenyekiti wa Tottenham kutaka kusubiri mpaka mashindano ya Euro yaishe ndo aongee na Kocha huyo wa Ufaransa kimemuudhi AVB na kuona ya kuwa hajapewa kipaumbele.

David Moyes nae alihusishwa kwamba angeweza kuwa kocha wa Tottenhama lakini alijiengua mwenyewe katika mbio hizo kwa kusema, “Nachoweza sema ni kuwa, Sijaongea na Tottenham na wala hawajanitafuta. Mie ni kocha wa Everton na kwa sasa nipo Poland nkiangalia wachezaji ambao naweza waongeza katika timu yangu ya Everton msimu ujao”.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 22, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: