Emmanuel Okwi kutimkia Ulaya


MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi, anatarajia kuondoka nchini wakati wowote baada ya kupata ofa nyingine kutoka kwenye nchi za Ubelgiji na Italia, ambapo tayari hatua za awali zimeanza kufanyika.
Okwi, ambaye hivi karibuni aliripotiwa kutakiwa na timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, hivi sasa amepata ofa nyingine kubwa kutoka kwenye klabu za Ulaya.

Akizungumza na Mtanzania Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa wanatarajia kuvuna kiasi cha euro laki nane baada ya kukamilika kwa mpango huo.

“Wapenzi wa Simba wanapaswa kufahamu kwamba Okwi hatutaweza kuwa naye katika msimu ujao wa Ligi Kuu, kwani tayari tumepata wakala wa uhakika ambaye anafanikisha mpango wa kumpeleka Italia au Ubelgiji.

“Mazungumzo yanaendelea vizuri na tunatarajia kuvuna kiasi cha euro laki nane, fedha ambayo itatumika kurekebisha kikosi na kufanyia masuala mengine kwa ajili ya kuiletea Simba maendeleo.

“Ni kweli anatakiwa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, lakini sisi tunatazama zaidi ukubwa wa ofa itakayokuja, tutakapokamilisha taratibu za uhamisho tutaweka wazi kila kitu kama ambavyo tulifanya wakati wa uhamisho wa Mbwana Samata kwenda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Achilia mbali michuano ya Ligi Kuu, kuna uwezekano pia tukamkosa kwenye michuano ya Kombe la Kagame, kutokana na jinsi mazungumzo yanavyoendelea,” alisema Kamwaga.

Okwi, ambaye ni mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Uganda, amekuwa kivutio kwa mawakala baada ya kuonyesha kiwango cha juu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufunga mabao muhimu wakati Simba ilipokuwa inawakilisha Taifa kwenye Kombe la Shirikisho.

Kamwaga pia alisema kuwa mpaka kufikia katikati ya msimu ujao wa Ligi, klabu ya Simba itakuwa inatumia uwanja wake wa mazoezi, kwani kuna hatua zinafanyika ili kukamilisha lengo hilo.

Simba hivi sasa inafanya mazoezi yake kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe, kujiandaa na michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

Chanzo: newhabari

Advertisements

Posted on June 22, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: