Ukanda wa Tenga waboronga Afcon 2013


UKANDA wa Afrika Mashariki na Kati ulio chini ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Cecafa, umeingiza timu mbili kuwania kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini mwakani.

Uganda, mabingwa wa soka ukanda huo na Ethiopia ndizo pekee zilizopenya hatua ya makundi baada ya kufanya vema mechi zao mwishoni mwa wiki.

Uganda iliitoa Congo kwa jumla ya mabao 5-3, ilishinda mabao 4-0 mjini Kampala baada ya kufungwa mabao 3-1 mjini Brazaville wakati Ethiopia ilitoka suluhu na Benin kabla ya kufungana bao 1-1 mjini Porto-Novo.

Tanzania iliyokuwa ikicheza na Msumbiji, ilitolewa kwa kufungwa penalti 7-6 baada ya sare mbili ya 1-1 ya Dar es Salaam na Maputo.

Rwanda ambayo iliibana Nigeria kwa suluhu katika mchezo wa kwanza, ilitandikwa mabao 2-0 mjini Abuja.
Zimbabwe ilifuzu kwa bao la ugenini baada ya kuilaza Burundi bao 1-0 mjini Harare baada ya kufungwa na Burundi 2-1 katika mchezo wa kwanza.

Nayo Togo iliitoa Kenya kwa kuifunga bao 1-0 ikiwa na faida ya bao la ugenini kwani katika mchezo wa kwanza, Kenya ilishinda mabao 2-1.

Timu zilizofuzu ni Algeria, Sierra Leone, Cameroon, Malawi, RD Congo, Cape Verde na Liberia wakati mechi ya Afrika ya Kati na Misri itapigwa Juni 30 kutokana na sababu mbalimbali za kiusalama.

Chanzo Mwananchi

Advertisements

Posted on June 19, 2012, in Bongo, Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: