Man Utd wamtaka Rodriguez kama kuziba pengo la Nani..


James Rodriguez (katikati)

Timu ya Manchester United inajiandaa kumnunu winga wa timu ya Porto James Rodriguez kama mbadala wa winga Nani ambaye anaonekana anaelkea kuihama klabu hiyo ya
Manchester.

Juventus ndio klabu ambayo inamfuatilia kwa karibu Nani na kitendo cha Manchester kutomuongezea mshahara winga huyo inapelekea kuongeza uwezekano wa mchezaji huyo kuhama. Mchezaji huyo amewaambia marafiki zake wa karibu ya kuwa ameudhika na kitendo cha Manchester kutompatia mkataba mpya na kukaa kimya mpaka sasa bila hata ya kumjibu chochote.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alikuwa ameomba kupandishiwa mshahara wake mpaka paundi 120,000 kwa wiki lakini mpaka sasa hakuna makubaliano yaliofanyika.

Manchester inamfuatilia kwa karibu Mkolombia Rodriduze na uvumi huo ndio unazidi weka matatani uwezekano wa Nani kubakia Man Utd msimu ujao.

Rodriguez mwenye umri wa miaka 20 amefunga magoli 13 katika mechi 20 alizicheza msimu uliopita.

Porto wamemuwekea kibandiko cha bei ya paundi mill 25 mchezaji huyo ambaye tayari ameshasema anataka kuichezea Man Utd.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 19, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: