Mabeki Yanga waanza kuliwaza benchi


BAADHI ya wachezaji wa Yanga wanaocheza nafasi ya beki wa kati namba nne na tano wameanza kuingiwa na mchecheto wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na uongozi kuendelea kusajili wachezaji wanaocheza nafasi hizo.

Hali hiyo imekuja hivi karibuni baada ya klabu hiyo kuwanasa mabeki wawili, Kelvin Yondani kutoka Simba na Ladislaus Mbogo wa Toto Africa.

Usajili wa wachezaji hao unaifanya Yanga kufikisha wachezaji saba ambao ni Chacha Marwa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Idd ‘Chuji’ Zuber Ubwa, Bakari Mbegu, Yondani pamoja na Mbogo.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti hivi karibuni, baadhi ya wachezaji hao (majina tunayo) walionekana kuwa na hofu ya kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Walisema kwa sasa wanachosubiri ni timu kuingia kambini kujiandaa na michuano ya Kagame na huko ndipo watakapopata majibu sahihi ya maswali yao.

“Siwezi kuzunguza lolote kwa sasa juu ya hali hiyo kwa sababu mimi siyo kocha lakini majibu yatajulikana baada ya kuingia kambini hivi karibuni.”

Kikosi hicho cha Yanga kinatarajia kuingia kambini leo kujiandaa na harakati zake za kutetea ubingwa wa mashindano ya Kagame ikiwa ni pamoja na mikikimikiki ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Posted on June 18, 2012, in Bongo, Mpira and tagged . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: