Liverpool wamtaka Beki wa Ujerumani..


Benedikt Howedes

Bosi wa Liverpool Brendan Rogers inasemekana anamtaka beki mwenye asili ya Ujerumani Benedikt Howedes na yupo tayari kutoa fedha kwa ajili ya kumpata beki huyo ili kuweza kuimarisha safu ya ulinzi wa liverpool.

Kocha huyo mpya wa Liverpool anawaswas na safu ya ulinzi iliyopo Liverpool hasahasa mabeki wa katikati. Martin Skrtel amekuwa ndo beki pekee wa kutegemewa huku mwenzake Daniel Agger akiwa akisumbuliwa na majeraha mara kwa mara na Mkongwe Jamie Carragher anatarajiwa kuwa  mchezaji wa akiba na sio wa kucheza kila mechi.

Beki huyo Howedes kwa sasa yupo na timu yake ya taifa ya Ujerumani katika mashindano ya Euro 2012 amewezachaguliwa kujiunga na timu hiyo kutokana na mchango wake alioutoa kwa timu yake ya Schalke na kuweza ifanya timu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu na hivyo kupelekea timu hiyo kupata nafasi ya kushiriki Champions League msimu ujao.

Mchezaji huyo amechezea klabu yake hiyo ya Schalke tokea alipokuwa na umri wa miaka 13 na kupelekea uvumi wa kuwa anaweza kuihama klabu hiyo msimu huu.

Chanzo: Caughtoffside

Advertisements

Posted on June 18, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: