Nani: Nalazimishwa kuondoka Man Utd.


Nani

Mreno huyo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake aliokuwa nao na Man Utd. Alikuwa anategemea ya kuwa angeweza kuongezewa mkataba mwingine ili aendelee bakia na miamba hiyo lakini habari imekuwa tofauti.

Mchezaji huyo anahofia ya kuwa Man Utd wanamfukuza kijanja klabuni hapo kwa kugoma kumpatia mkataba mpya.

Maongezi ya mkataba mpya hayafanyiki tena ingawaje mchezaji huyo amejaribu kupunguza maombi ya mshahara wake mara mbili ili tu aweze bakia klabuni hapo lakini Man Utd wala hawaoneshi mpango wa kutaka kumpa mkataba huo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaanza dhania na kuamini ya kuwa Man Utd wanataka kumuuza wakati bei yake bado ipo juu ndo maana hawataki mpa mkataba mwingine.

Ferguson ana wachezaji kama Ashley Young na Antonio Valencia wa kuweza cheza kama mawinga kwa hiyo umuhimu wa mchezaji Nani haupo.

Nani alitua Man Utd akitokea Sporting Lisbon kwa ada ya paundi mill 25 mwaka 2007 na Man Utd ikiamua kumuuza kama inavyodhaniwa basi atauzwa kwa hela nyingi zaidi ya aliyonunuliwa.

Chanzo: Dailymirror  

Advertisements

Posted on June 17, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: