Hatimaye Van Persie kuuzwa..


Van Persie

Arsenal wamemuwekea kibandiko cha bei mshambuliaji wao Robin van Persie cha paundi mill 30.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Uholanzi hajakubali kusaini mkataba mpya mpaka sasa huku akiwa amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake.

Arsenal wapo tayari kuupandisha mshahara wa mchezaji huyo mpaka paundi 130,000 kwa wiki lakini bado mchezaji huyo anaendelea kusita kusaini mkataba huo mpya.

Mwenyekiti wa Arsenal Peter HilloWood amesema kama kuna klabunyingine ikija na ofa ya kumlipa van Persie mshahara wa paundi 250,000 kwa wiki basi hapo itabidi Arsenal wamuachie mchezaji huyo kwa mshahara huo ni mkubwa sana na hao kama klabu hawapo tayari kuutoa.

Arsenal bado hawajakata tamaa ya kumbakiza mchezaji huyo lakini kama nahodha huyo wa Arsenal akilazimisha kuhama basi Arsenal haitomzuia.

Klabu kubwa nyingi zamfuatilia mchezaji huyo zikiwemo Man City, Juventus na PSG.

Huku timu ya kitajiri ya Anzhi inayoongozwa na Guus Hiddink ipo tayari kutoa ofa yoyote kwa ajili ya mchezaji huyo.

Kama hapatokuwa na timu itakayofikia paundi mill 30 basi Arsene Wenger atakuwa tayari kumbakiza mchezaji huyo mpaka mwaka 2013 ambako ndipo mkataba wake unapoishia na kumfanya mchezaji huyo kuwa huru na kujiunga na klabu yoyote ile aitakayo.

Chanzo: Dailymirror

Advertisements

Posted on June 17, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: