UEFA wawaadhibu Crotia kwa ubaguzi dhidi ya Balotelli.


Mario Balotelli

Uefa imeamua kulivalia njuga swala la kuzomea kama Nyani katika mechi dhidi Crotia na Italia na hivyo kuamua kukiadhibu chama cha mpira cha nchini Crotia.

Uefa wametangaza ya kuwa  wanawachukulia adhabu chama hicho cha Crotia kutokana na ubaguzi uliofanywa na mashabiki wao dhidi ya Balotelli.

Haijajulikana bado kama adhabu hiyo itajumuisha na kesi ya kutupwa kwa ndizi uwanjani. Ambao utupaji huo ukimlenga Balotelli kuwa yeye ni nyani na ndizi ndio chakula chake.

“UEFA wamefungua kesi dhidi ya shirikisho la mpira la Croatia kutokana na fujo zilizofanya na mashabiki wao walio kuwa wakurusha baruti na kufanya ubaguzi katika mechi dhidi ya Italia. Bodi inayohusika na swala hilo itasikiliza hiyo kesi tarehe 19 mwezi wa 6″walisema UEFA.

Mchezaji huyo wa Man City ambaye mwanzoni alishasema ya kuwa kwa yeyeto atakaye mletea maswala ya ubaguzi basi atakufa nae.. Lakini kwa bahati mbaya ubaguzi ndo huo ameshafanyiwa…

Croatia

Kundi liitwalo FARE (Football Against Racism in Europe) ambalo ni kundi dhidi ya ubaguzi ndilo lililotoa ushahidi wa ubaguzi huo kwa kusema kupitia Twitter ya kuwa, ” wafuatiliaji wa FARE anadhihirisha ya kuwa kati ya mashabiki 300 mpaka 500 wa Crotia walihusika katika kumtukana Mario Balotelli kutoka na rangi yake jana usiku mjini Poznan”.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika and tagged , , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: