Swansea wamemtangaza Mdenmark Michael Laudrup kama Meneja (kocha) wao mpya.


Michael Laudrup

Laudrup amechukua nafasi ya Brendan Rodgers ambaye amehamia Liverpool.

Kocha huyo mpya wa Swansea ambaye ameshawahi zifundisha klabu za Brondby, Getafe, Spartak Moscow na Real Mallorca amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Swansea.

Graeme Jones ambaye ni kocha msaidizi wa Roberto Martinez alikuwa nae anafuatiliwa ili awe kocha lakini mwishowe alikataa ofa hiyo na Laudrup kuwa ndo mgombaniaji pekee.

Inasemekana kuchaguliwa kwa kocha huyo ambaye pindi alipokuwa mchezaji alishinda mataji mengi akiwa na klabu za Barcelona, Real Madrid, Juventus n Ajax ni kwa ajili ya kuwapa ari wachezaji hao wa Swansea na pia kuendeleza Staili ya kumiliki mpira.

“Ninafuraha kuwa hapa na nategemea ya kuwa utakuwa mwanzo mzuri wa mafanikio. Niliongea na watu wengi kuhusu Swansea na pia nkaangalia DVD kabla ya kujiunga nao.Kila mtu anajua staili ya mpira ambayo Swansea wanacheza na haina tofauti na mie ninavyo fundisha.

HISTORIA YA LAUDRUP..

1964: Alizaliwa Juni 15 Frederiksberg,Denmark.

1981: Acheza mechi yake ya kwanza katika ligi akiwa na timu ya KB.

1982: Arudi timu yake ya utotoni Brondby na kuisaidia kupanda daraja, huku akifunga magoli 15 na kutangazwa mchezaji bora wa mwaka wa Denmark.

1983: Ajiunga na Juventus ambao wamtoa kwa mkopo kwenda Lazio.

1985: Arudi Juve na atangazwa mchezaji bora wa Denmark kwa mara ya pili.

1986: Aisaidia Juve kushinda  ligi na Intercontinental Cup.

1989: Ajiunga na Barcelona chini ya kocha Johan Cruyff’s

1991: Ashinda vikombe vinne mfululizo na Barcelona.

1992: Aisaidia Barca kushinda kombe la UEFA.

1994: Ajiunga na Madrid.

1995: Aisaidia Madrid ipiku Barca na kuifanya kutwaa kombe la ligi.

1996: Ajiunga na Vissel katika ligi ya Japan.

1997: Ajiunga na Ajax na kuisaidia kushinda ligi.

1998: Aiongoza Denmark katika kombe la dunia mpaka robo fainali.

2000: Awa kocha msaidizi wa Denmark.

2002: Awa kocha wa Brondby na kuifanya twaa kombe katika mwaka wa kwanza.

2005: Brondby washinda tena vikombe viwili.

2006: Brondby wamaliza ligi nafasi ya pili.

2007: Awa kocha Getafe na kuipeleka klabu mpaka fainali ya Copa del rey.

2008: Ajiunga na Spartak Moscow.

2009: Afukuzwa ukocha Spartak Moscow.

2010: Ajiunga na Real Mallorca na kuisaidia kutoshuka daraja.

2011: Aachia ngazi Mallorca.

2012: Ajiunga na Swansea kwa mkataba wa miaka miwili.

Chanzo: Dailymail

Advertisements

Posted on June 16, 2012, in Mpira, Mpira kwa Dakika, Tetesi and tagged , . Bookmark the permalink. Leave a comment.

Comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: